Ripoti
ya Benki ya dunia kuhusu chakula barani Afrika inasema kuwa wakulima
wanaweza tu kuzalisha chakula cha kutosha kulisha watu wa bara hilo
ikiwa vikwazo vya biashara kati ya nchi hizo vitapunguzwa.
Mamilioni ya watu katika eneo la Sahel wanakumbwa na njaa na utapia mlo.
Kwa
mujibu wa benki hiyo, tatizo la uhaba wa chakula litapunguka tu ikiwa
wakulima katika maeneo yenye kuzalisha chakua wataweza kuruhusiwa
kusafirisha mazao yao kupitia mipaka bila malipo.
Kuondoa vikwazo vya mipakani, pia itapunguza gharama ya chakula.
Benki
ya dunia inasema kuwa asilimia tano ya nafaka barani Afrika inatoka
katika mataifa mengine ya Afrika ikisema kuwa mashamba makubwa yenye
dhoruba hayatumiwi kwa upanzi.
Je hii ndio sababu ya uhaba wa chakula Afrika kweli? Toa maoni yako.........
0 comments:
Post a Comment