Tume inayoendesha uchunguzi kuhusiana na vifo vya wachimba migodi
katika machimbo ya Marikana nchini Afrika kusini, inatarajiwa kurejelea
vikao vyake wakati wowote kuanzia sasa.
Vikao
hivyo vilisitishwa mapema mwezi huu ili familia za wale waliofariki
wakati wa vurugu za Marikana kusafiri kwenda kusikiliza vikao hivyo.
Wengi wao wanaishi mamia ya kilomita mbali na ambako tume hiyo inaendesha vikao vyake.
Mnamo
mwezi Agosti Polisi iliwafyatulia risasi waandamanji katika mgodi huo
na kuwaua wachimba migodi 34,baada ya vurugu kuzuka katika maandamano
hayo.
chanzo cha habari : BBC
0 comments:
Post a Comment