Wakizungumza na waandishi wa
habari sokoni hapo kwa hasira, baadhi ya wafanyabiashara hao waliokosa maeneo
ya kuuzia na matokeo yake kuuza nje ya soko huku wakifukuzwa mara kwa mara na
mgambo wa jiji, walisema kuwa ndani ya soko kuna baadhi ya maeneo yameshikwa na
watu wasio wamachinga.
“Kama mnavyoona ndugu
waandishi, ndani ya soko kuna baadhi ya maeneo yako wazi (hayatumiki) lakini
sio kama hayana watu, kuna watu lakini siyo wamachinga
bali wametoka mbali na kushika maeneo ndani ya soko huku wahusika tunauza nje
baada ya kukosa maeneo huko ndani ya soko” alisema mmoja wao Scola Clement, na
kuongeza
“Pia ugawaji wa meneo haya
kulitawaliwa sana na rushwa kwani katika ugawaji wa maeneo ukiwa na mkono mfupi(
usipotoa hela) hutapewa eneo bali utazungushwa hadi utaamua mwenyewe kutoa hela
upate eneo baada ya kushuhudia mwenzako aliyetoa hela amepewa eneo haraka,
mbali na hilo pia katika kugawa maeneo haya siyo yote yalikuwa wazi bali kuna
baadhi yalikwisha gawiwa kabla hata ya tangazo rasmi kutoka”
Aliongeza kwa kusema kuwa
“baada ya tangazo kutoka tulipoenda kushika maeneo baadhi ya maeneo tuliambiwa
yamekwisha chukuliwa wakati ndio siku ya kwanza tena alfajiri, matokeo yake leo
hii yale maeneo tuliyokuwa tunaambiwa yamekwisha chukuliwa leo wahusika ambao
ni wafanyabiashara wakubwa mijini na wengine ni wa masoko mengine wanatuuzia
yale maeneo kwa shilingi laki tatu(300,000) kama siyo walipewa maeneo haya kwa
rushwa ni nini” alihoji.
Mfanya biashara mwingine
aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Hamis alizidi kusisitiza kuwa rushwa
ilitawala katika ugawaji wa maeneo hayo “mimi kama mimi naamini rushwa
ilitawala sana kwani mbali na baadhi ya maeneo kupewa watu ambao siyo wahusika
na leo kuja kutuuzia, pia kuna baadhi ya watu wamepewa maeneo makubwa ya
mabanda mawili na zaidi, wengine madogo ya banda moja huku wengine wakipewa
eneo lisilotosha hata kibanda 1”
Mussa alisema kuwa pamoja na
halmashauri ya jiji kusikia kilio chao cha kupatiwa eneo la kufanyia biashara
na kupewa eneo hilo lakini bado wako hatarini
kupata magonjwa ya mlipuko hasa katika msimu huu wanaotarajia mvua, nah ii ni
kutokana na soko hilo
kutokuwa na huduma muhimu za kijamii na miundombinu huku wakiambulia kuahidiwa
bila utekelezaji.
Aliongeza kuwa soko hilo
jipya ni sawa na voda fasta kwani halikuwa na maandalizi yoyote kimiundombinu
ikiwemo dampo kwa ajili ya taka zinazozalishwa sokoni hapo, choo, maji safi,
pia hadi sasa hakuna ulinzi wa mali zao na wateja wao, ambapo pia alilalamikia
swala la lango kuwa moja linalotagemewa kwa kutoka na kuingia sokoni hapo
ambapo huhatarisha maisha ya wafanyabiashara hao pindi janga likitokea.
Akijibu tuhuma hizo afisa
habari wa halmashauri ya jiji la Arusha, Ntagenjwa Hoseah alikanusha vikali
ugawaji wa maeneo katika soko hilo kuhusishwa na maswala ya rushwa ambapo
katika swala la miundombinu alisema kuwa halmashauri iko katika maboresho ya
miundombinu ya soko hilo huku akisema kuwa kwa sasa wafanyabiashara hao
wanatumia choo cha soko la krokon lililoko pembezoni mwa soko hilo jipya la
NMC.
0 comments:
Post a Comment