Kundi
la wachunguzi wa haki za kibinadam la umoja wa mataifa limewasilisha
rasmi ombi la kukutana na Rais wa Syria Basher al Assad kwa mara ya
kwanza tangu Majeshi yake yaanze kupigana na wanamgambo wanaotaka
kuipindua serikali yake .
Kundi hili
linalongozwa na aliyekuwa kiongozi wa wapelelezi wa umoja huo, Carl del
Ponte limesema lina jukumu la kushughulikia makosa mengi tu ya jinai
ambayo yamefanyika .
Wakati huohuo
serikali ya syria imetangaza kukubali
kusitisha mapigano dhidi ya waasi kwa kipindi cha siku nne ili
kuwaruhusu wasyria kuadhimisha sikukuu ya Eid ul Adha kuanzia leo siku ya ijumaa .
Awali, Habari za maafikiano ya kusitisha mapigano zilitangazwa hivi karibuni na mpatanashi wa umoja wa mataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi.
Lakini
jeshi la taifa hilo likataka kutangazwa rasmi kwa amri hiyo ya
kusitishwa mapigano ikidai muda zaidi kutathmini athari kwa pande zote
mbili katika mzozo huu.
0 comments:
Post a Comment