Watoto wanaotoka katika mazingira
magumu na kulelewa katika vituo maalumu, wameiomba serikali kuangalia uwezekano
wa kuwaondoa watoto wenzao wanaoishi magerezani na mama zao bila hatia ,kwani
licha ya kuteseka na hali mbaya ya mazingira iliyopo gerezani, wanakosa mahitaji
ya msingi yanayomstahili mtoto kuyapata.
Aidha wamedai kuwa kitendo cha
watoto hao kuendelea kuishi gerezani ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata
elimu na haki zingine wakati hawana hatia yoyote hivyo wameililia
serikali iwatoe na kuwakabidhi hata kwenye vituo vya kulelea watoto .
Watoto hao walitoa kilio hicho
mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha ,Magesa Mulongo aliyekuwa mgeni rasmi katika
harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa mawili katika kituo cha St.Gemma
kilichopo kisongo jijini hapa, ambacho ni kituo pekee Tanzania kinacholea watoto
waliopo gerezani ambao mama zao walifungwa.
Wakisoma risala yao kwa pamoja
iliowasisimua wageni mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo huku baadhi yao
kujikuta wakibubujikwa na machozi akiwemo mkuu huyo wa mkoa,watoto hao wenye
umri mdogo walisema kuwa kitendo cha wenzao kukaa gerezani kama wafungwa ni
kuwanyima uhuru wa kuishi kwani hawana hatia wenye hatia ni wazazi ama walezi
wao.
Waliendelea kusema ni vizuri
serikali ikatafakari upya na kuona umuhimu wa kuwaondoa watoto hao waliopo
magerezani ili waungane na wenzao waliopo uraiani na kuondokana na mateso
wanayoyapata bila hatia ikiwemo kuathirika kisaikolojia kutokana na mazingira ya
mageraza pamoja na kukosa elimu.
‘’kwanini serikali inatufunga
gerezani kwani tumekosa nini kama ni kosa wametenda wazazi wetu sisi tunafanya
nini gerezani ,watoto wanashindwa kusoma ,kula vizuri na kucheza na wenzao,
viongozi wa serikali tuoneeni huruma jamani, tunaomba wenzetu watolewe
gerezani’’walisema.
Naye meneja wa kituo hicho,Flora
Ndwata alisema kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka 2007 kikiwa na watoto watatu
, hadi sasa kina jumla ya watoto 14 wenye umri wa miaka mitatu hadi 10 na kwamba
kimeshindwa kuchukuwa watoto wengi kwa sababu ya kukosa fedha za
kujiendeshea.
Alisema kituo hicho kilibuniwa na
masister wa kanisa katoliki,shirika la St Gemme baada ya masister hao kuguswa na
hali mbaya za watoto hao waliopo magerezani na kuamua kuanzisha mkakati wa
kuwasaidia kwa kuwaondoa kwa wazazi wao waliopo gerezani.
Alisema hatua hiyo iliwafanya
wachangishane na kuamua kujenga vyumba viwili ambapo walifanikiwa kuwa na watoto
wawili ambao walimudu kuwalea na baadae watu mbalimbali waliwaunga mkono kwa
kuwasaidai michango iliyosaidia kuongezeka kwa watoto hao.
''tumekuwa
tukiwauliza wamewapataje watoto hao wanasema wengine waliingia gerezani wakiwa
na ujauzito na wengine walisema walipata ujauzito wakiwa huko na
kujifungua''alisema Sister Flora
Aliongeza kuwa hadi sasa wana
watoto kutoka gereza kuu la Isanga Dodoma,gereza la Babati na gereza kuu la
Kisongo jijini hapa na kwamba wanatarajia kuomba watoto wengine kadri wanapo
kuwa na uwezo wa kuwahudumia.
Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa
Arusha,Magesa Mulongo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwanye harambee hiyo ya
kuchangia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa,alifanikiwa kuchangisha shilingi
milioni 63.3 na kuvuka malengo ya shilingi milioni 46 zilizokuwa
zikihitajika,huku ofisi yake ikichangia shilingi milioni 10.
Wengine waliochangia ni pamoja na
mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongela ambaye alichangia shilingi milioni 1pamoja
na malori 9 ya mchanga na kokoto,kaimu mkurugenzi jiji la Arusha,Omari Mkombole
shilingi milioni 10.3,Mkurugenzi Rich Hotel Joseph Masawe shilingi milioni
2.5.
|
Home
»
»Unlabelled
» WATOTO WALILIA WENZAO WALIOKO GEREZANI
Wednesday, October 17, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment