Madiwani la halmashasuri ya
Arusha wametishia kususia shughuli zote
za maendeleo endapo mkurugenzi wa halmashauri hiyo halipha Idda hatawaonya na
ikiwezekana kuwachukulia hatua kali za kisheria wakuu wa idara katika
halmashauri hiyo kwa madai kuwa wanafanya shughuli zao huku wakikiuka sheria
kanuni na Taratibu za nchi.
Madiwani hao wamesema hayo
kwenye mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri
hiyo ambapo wamesema kuwa wakuu wa idara mbalimbali hasa idara ya kilimo na
fedha wamekuwa wakifanya kazi zao kinyume na taratibu hali inayohatarisha
maendeleo ya halmashauri hiyo.
Walisema kuwa endapo
mkurugenzi hatachukua hatua zozote hawako tayari kuumia kwa ajili ya
kuwanufaisha watu wachache huku wananchi wakikosa imani na serikali yao kwa ajili ya baadhi ya watu wanaotanguliza matumbo yao na kuwafanyia madudu
wananchi.
Walisema kuwa mara nyingi
madiwani wamekuwa wakibuni miradi mbalimbali za kimaendeleo kwa wananchi wao
lakini pindi ifikapo kwa mkuu wa idara hukataa endapo haina maslahi kwao hali
inayorudisha nyuma maendeleo ya kata husika kwa wananchi wake kukata tamaa
ambapo hali hiyo husababisha migogoro baina ya watumishi na wakuu hao kutokana
na madiwani kutaka kulinda kura zao kwa kutetea miradi hiyo ikubalike.
Mbali na hilo
pia waliwatuhumu idara ya fedha na kamati yake kwa kutowasilisha mahesabu ya
uhakika kwani hesabu hizo hudhiirisha kila aina ya ubadhirifu hali inayowafanya madiwani hao kumtaka
mkurugenzi kufuatilia swal hilo
kwa ukaribu.
Pia walisema kuwa mbali na
ubadhirifu wa fedha pia ardhi imekuwa ikigawanywa bila utaratibu unaojulikana
wala kuwepo kwa ripoti zake hali inayoonyesha manufaa hayo yanabaki mikononi
mwa wahusika wa idara ya ardhi
Kwa upande wake mkurugenzi wa
halmashauri ya Arusha Halipha Idda aliwaahidi madiwani hao kushughulikia swala hilo kwa kuwahoji
watuhumiwa katika vikao vya ndani kuelezea hayo ambapo ikionekana ripoti zao
zina kasoro au tuhuma hizo zina ukweli ndani yake atawachukulia hatua kali za
kisheria wabadhirifu wa fedha za serikali.
Mbali na hilo
pia aliwataka madiwani hao kuendelea kubuni miradi mbali mbali ya kuongeza pato
la halmashauri kwa ajili ya maendeleo yao kwani
wamekuwa wakitegemea fedha za serikali lakini zimekuwa zikichelewa sana na kukwamisha
maendeleo ambapo alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuwahisha fedha za
maendeleo kwani wamekwama kwa sehemu kubwa.
baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Arusha wakisikiliza kwa makini mmoja wao akiwasilisha hoja yake barazani hapo |
0 comments:
Post a Comment