KANISA la Kiinjili la Kilutheri
Kanisa
Akizungumza katika ibada maalumu na kutoa salaamu za maaskofu wa kanisa hilo nchini kote kuhusiana na matukio ya kuchoma moto makanisa ya Kikristo, iliyofanyika katika kanisa la jimbo kuu Kusini Mbagala, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, alisema kuwa wamekutana kwa madhumuni ya kuonyesha majonzi yao kwa vitendo vya uvunjifu wa amani walivyoviita ni kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa Watanzania.
Shao pia alisema kuwa madhumuni mengine ni kupokea matumaini ya
Aidha alisema kuwa katika ujio wa maaskofu 19 kutoka dayosisi mbalimbali za
Pia alisema kuwa hawakubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba
Askofu Shao alifananisha kuwa kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari ambayo mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema imezaa magugu yanayozaa matunda machungu.
Pia alilaani matumizi mabaya ya baadhi ya vyombo vya habari vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini huku vikifumbiwa macho na vyombo vya dola.
“Uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na kwa Watanzania wote wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi,” alisema.
Alihoji kuwa ni uvumilivu gani wakati wanashuhudia makanisa yakichomwa
Shao alisema kuwa uvumilivu wa Wakristo umetafsiriwa kuwa unyonge na woga na kufafanua kuwa wanyonge na waoga hufika wakati wakasema basi pale wanapodhalilishwa kupita kiasi.
Naye Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa, aliwataka Wakristo kuwa watulivu na kufunga na kuomba ikiwemo kuonyesha upendo.
Kanisa
Katika hatua nyingine kanisa la Faraja International Gospel, limechomwa moto na watu wasiofahamika na kusababisha hasara ya sh milioni 5.8.
Mchungaji wa kanisa
LHRC waonya
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeitaka serikali kuitisha mkutano wa dharura na viongozi wa dini zote ili kukomesha vitendo vinavyoendelea vya uvunjifu wa amani kwa kutumia imani za kidini.
Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba, katika tamko lao kuhusu ghasia zilizotokea Mbagala kutokana na imani za dini na mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Kijo-Bisimba alisema katika mkutano huo, serikali inapaswa kushauriana na viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wao kuwa na uvumilivu wa kidini ili wasije wakalifikisha taifa katika machafuko.
Aidha alitaka kukemewa kwa nguvu zote utumiaji wa propaganda ya udini katika siasa za ndani kwani inawagawa Watanzania na kuyumbisha demokrasia ya kweli.
“Hili suala la kuchanganya siasa na dini tumeshawahi kukemea katika ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2010 kwani tulishaona propaganda hizi za kidini zilitumika
Hata hivyo hakuna jitihada zozote zilizofanywa kukomesha kuhusisha siasa na dini jambo ambalo ni hatari
Pia kituo hicho kimevitaka vyombo vya dola kuchukuwa hatua za tahadhari pale ambapo kuna mijadala ya wazi inayochochea chuki na kuhatarisha amani na utulivu wa nnchi.
Akigeukia mauaji ya Kamanda Liberatus Barlow, alisema walichokibaini ni kwamba jamii inaendeleza tabia ya kujichukulia sheria mikononi hali inayohatarisha amani na utulivu wa nchi.
0 comments:
Post a Comment