CHAMA cha demokrasia na maendeleo(Chadema) ngazi ya taifa kimelazimika kuunda tume ya kuchunguza tuhuma mbalimbali za matumizi mabaya ya fedha za chama hicho mkoani Arusha sanjari na migogoro mbalimbali inayofukuta chini kwa chini ndani ya chama hicho mkoani hapa.
Baadhi
ya wajumbe
waliotajwa kuunda tume hiyo ni pamoja na wabunge wa Chadema akiwemo
mbunge wa
viti maalumu mkoani Kilimanjaro ,Grace Kiwhelu,mkurugenzi wa halmashauri
na bunge,John Mrema sanjari na katibu wa mbunge wa Moshi mjini,Basil
Lema.
Kwa mujibu
wa vyanzo vya habari vilivyotufikia vimedai kwamba uamuzi wa kuunda
tume hiyo umekuja baada ya uongozi wa Chadema ngazi ya taifa kupokea lawama
mbalimbali kuhusu matumizi mabaya fedha za chama hicho zikiwemo zile za
rambirambi za wahanga wa mauaji ya najuari 5 mwaka jana waliouwawa katika
maandamano ya Chadema.
Itakumbukwa
ya kwamba hivi karibuni tuliripoti habari za mjane,Asia Ismail
ambaye marehemu mme wake aliuwawa katika maandamano ya januari 5 mwaka jana
ambapo mjane huyo alikishutumu chama hicho kutafuna fedha za rambirambi
zilichochangwa katika uwanja wa NMC huku akidai kwamba aliambulia zile
zilizotolewa na kada maarufu wa CCM nchini,Mustafa Sabodo.
Vyanzo hivyo
vya habari vimetuambia kuwa tume hiyo itawasili wiki hii mkoani
Arusha kwa lengo la kuchunguza madai hayo ambapo itakutana na viongozi kadhaa
wa Chadema mkoani hapa wakiwemo makada
mbalimbali.
Vyanzo hivyo
vimesema kwamba tume hiyo pia itachunguza tuhuma za mbunge
wa zamani wa jimbo la Arusha
mjini,Godbless Lema kudaiwa kuvuruga chama hicho mkoani hapa ikiwa ni pamoja na kuingilia maamuzi mbalimbali
yanayotolewa na viongozi wa chama hicho katika ngazi za wilaya na mkoa.
Hatahivyo,vyanzo
hivyo vya habari vilienda mbali zaidi na kudai kwamba uamuzi wa kutuma tume
hiyo mkoani hapa ulifuatia baada ya vigogo wa Chadema wakiwemo baadhi ya
wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho
kutoridhishwa na hali ya mwenendo
wa chama hicho mkoani hapa huku wakidai kwamba endapo tuhuma hizo zikifumbiwa
macho zitakipelekea chama hicho kupoteza mvuto mbele ya wanachama wake.
“Uamuzi wa
kutuma tume hii ulitokana baada ya makao makuu kupokea tuhuma mbalimbali za
matumizi mabaya ya fedha za chama hapa Arusha na mifarakano ya chini kwa chini ndani
ya Chadema mkoani hapa”kilisema chanzo cha habari
Mmoja wa
wajumbe walioteuliwa ndani ya tume
hiyo(jina limehifadhiwa kwa sasa) amekaririwa akiwaambia baadhi ya wanachama wa
Chadema mkoani Arusha kwamba hawakutarajia mkoa wa Arusha kama ungeingia katika hali ya mtafaruku na kukabiliwa na
tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
Akihojiwa na waandishi wa habari, katibu wa Chadema mkoani Arusha,Aman Gorugwa alikanusha madai hayo
na kusema kwamba hakuna tume inakuja Arusha kuchunguza tuhuma yoyote na
viongozi waliotajwa wanakuja mkoani hapa kuongeza nguvu za kampeni katika
uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Daraja mbili.
Alisisitiza
kwamba huenda baadhi ya makada wa Chadema mkoani hapa wameamua kutumia jukwaa
la viongozi wanaokuja mkoani hapa kuwapatia orodha ya tuhuma wanazotaka
ziwafikie na kuwashangaa kwa kuwaita mamluki huku akihoji ni kwanini
hawakuzifikisha mbele ya uongozi wa chama mkoani hapa.
Na Woinde Shizza
0 comments:
Post a Comment