.
kiongozi wa mpito wa Libya, Mohamed Magarief alipokuwa akiongea na waandishi wa habari |
Kiongozi
wa mpito wa Libya, Mohammed Magarief, amesema kuwa mwaka mmoja baada ya
Kanali Gaddafi kuuwawa, nchi bado haijakombolewa kikamilifu.
Bwana
Magarief - ambaye anaongoza bunge - alitoa mfano wa hali katika mji wa
Bani Walid, shina la Gaddafi, ambako hivi karibuni kumetokea mapambano
baina ya wapiganaji wanaounga mkono serikali na wale wanaoshukiwa kuwa
wafuasi wa Gaddafi.
Bwana Magarief piya
alisema kuchelewa kufanya mabadiliko ya idara ya sheria na kuunda jeshi
na kikosi cha polisi rasmi, pamoja na kushindwa kuwanyang'anya silaha
wapiganaji, kunazidisha wasiwasi.
chanzo cha habari BBC
0 comments:
Post a Comment