Aliyetangazwa kuwa askofu mkuu wa kanisa Anglikana Cantebery na ambaye
amethibitishwa hii leo, Justin Welby amesema ameshangazwa sana na
wadhifa aliopewa wa kuliongoza kanisa hilo.
Katika
mkutano na waandishi wa habari, Askofu Justin Welby ambaye ni askofu wa
Durham, alielezea msimamo wake wa kuunga mkono kutawazwa kwa wanawake
kama maaskofu.
Aliongeza
kuwa watu watu hawapaswi kuwanyanyapa wapenzi wa jinsia moja kanisani,
lakini akakiri kuna mgawanyiko kanisani kuhusu ndoa za jinsia moja.
Welby
aliyefanya kazi katika sekta ya mafuta , anaonekana kama mhafidhina kwa
mrengo wa kanisa hilo ambalo linaegemea upande wa kiivanjelisti.
Ataanza kazi yake mwezi Machi mwaka ujao baada ya Askfo mkuu Rowan
Williams kuachia ngazi.
Baada ya uteuzi wa
Askofu mkuu Justin Welby kuwa mkuu wa Kanisa la Anglikana, viongozi
mbalimbali wa kanisa hilo wamezungumzia uteuzi huo.
Baadhi ya maaskofu wa nchi mbali mbali wa makanisa ya Kianglikana akiwemo wa Nigeria na Tanzani askofu Mokiwa wamepinga vikali kanisa kutetea mapenzi ya jinsia moja
0 comments:
Post a Comment