Wanavijiji nchini Kenya kaskazini wanahofia kuzuka
kwa mapigano zaidi baada ya takriban polisi 29 kuuwawa mwishoni mwa
wiki.
Polisi hao walivamiwa walipokuwa wanajaribu kurudisha ng'ombe waliokuwa wameibwa.
"Hali
ni ya wasiwasi sana, huku walinda usalama waliojihami kwa silaha
wakipiga doria vijijini," kiongozi mmoja wa kidini huko Kaunti ya
Samburu alisema.
"Tunahofia kwamba maafisa
wa ulinzi waliojawa na hasira huenda wakawashambulia wananchi wasio na
hatia kwani waliowaua polisi hao wameshatoroka," alidokeza kiongozi
huyo.
Aidha alisema kwamba kungali kuna miili mingine ambayo haijapatikana.
Wasamburu na Waturkana huibiana mifugo mara kwa mara. Pia hupigania maeneo ya lishe kwa mifugo na maji.
Kulingana na waandishi habari wa Kenya, majuma mawili yaliyopita watu 12 waliuwawa katika tukio kama hilo karibu na mahala hapo.
chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment