Mapigano yaendelea Gaza
Mapigano yameendelea usiku kucha katika eneo la Gaza licha ya fununu kuwa kumewekwa mkataba wa kusitisha mashambulio.
Israel inadaiwa kuendeleza mashambulio hayo katika maeneo kadhaa ya Gaza yaliyosababisha kupoteza kwa nguvu za umeme.
Takriban wapalestina ishirini wameripotiwa kuuawa .
Takriban wapalestina ishirini wameripotiwa kuuawa .
Hapo jana Israel ilisambaza ilani kuwaonya wakaazi waliokuwa pembezoni mwa Gaza, wahamia katikati mwa jiji kwa usalama wao.
Isarel imesema kuwa wapiganaji wa kipalestina wamerusha zaidi ya makombora mia na hamsini kwenye ardhi yake tangia Jumanne.
.......XXX...............XXX...........XXXMkewe Gbagbo kufikishwa the Haque
Mahakama
ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa mke wa
aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi Simone, Gbagbo.
Bi
Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa
vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya uchaguzi wa urais
nchini humo.
Mumewe
tayari amekamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo
iliyoko The Haque, kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.
Takriban watu 3,000 waliuawa kwenye machafuko yaliyotokea baada ya ya Gbagbo kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Gbagbo na mkewe walikamatwa ndani ya handaki moja Aprili mwaka wa 2011, miezi mitano, baada ya uchaguzi wa urais.
Wanajeshi
wa rais wa sasa wakiungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa
walianzisha msako mkali dhidi yao, baada ya kujificha ndani ya ikulu ya
rais.
anatuhumiwa kuhusika na mauaji,
ubakaji, dhuluma na ngona na kuwadhulumu wapinzani wa serikali miongoni
mwa mashtaka mengine mjini Abidjan.
Licha
ya kuwa Bi Gbagbo hakuwa akiwania kiti chochote cha kisiasa, ripoti
zinasema kuwa alikuwa na mamlaka makubwa na kuwa alimshawishi mumeo
kutokubali matokeo ya uchaguzi.
Gbagbo,
67, alihamishwa hadi The Haque mwaka uliopita, na kuandikisha historia
ya kuwa rais anayeondoka wa kwanza kufikishwa mbele ya mahakama hiyo ya
ICC.
Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo yote.
Kabla
ya kuhamishwa hadi the Haque, Gbagbo na mkewe mwenye umri wa miaka 63,
walifunguliwa mashtaka nchini Ivory Coast kuhusiana na uhalifu wa
kiuchumi, ikiwemo mdai ya kupora mali, wizi wa nguvu na kutumia
rasilimali za umma kwa njia mbaya
.........xxx...........xxx............xxx.............
Jaribio la mapinduzi yatibuliwa Sudan
Watu
kadhaa wamekamatwa na serikali ya Sudan, wakiwemo mkurugenzi mkuu wa
zamani wa idara ya ujasusi, Salah Gosh na maafisa kadhaa wa jeshi la
nchi hiyo kufuatia madai ya kujaribu kupindua serikali ya nchi hiyo.
Raia
kadha wamesema wameona magari kadhaa ya kivita na wanajeshi wakishika
doria katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
Katika
miezi ya hivi karibuni, Utawala wa Khartoum umeshuhudia kuongezeka kwa
maandamano dhidi ya serikali, kupinga kuongezeka kwa bei ya chukula na
pia kushinikiza mabadiliko ya kisiasa.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir amekuwa madarakani tangu mapinduzi ya serikali mwaka wa 1989.
Waziri wa habari wa Sudan Ahmed Belal Osman, amesema watu 13, wamekamatwa kuhusiana na njama hiyo ya kupindua serikali.
chanzo:bbc
0 comments:
Post a Comment