Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya
na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata Kaaya Cheti cha Udaktari
wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na
Chuo hicho mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika
kuendeleza Sekta ya Afya nchini. Sherehe hiyo fupi ilifanyika leo
Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Prof. Ephata
Kaaya akisoma risala kabla ya kumkabidhi Rais Kikwete Cheti cha
Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada
aliyotunukiwa na Chuo Desemba mwaka 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais
Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini leo Novermba 23, 2012
Ikulu jijini Dar es salaam..
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Ardhi
Prof Anna Tibaijuka, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein
Mwinyi na viongozi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
baada ya kukabidhiwa Cheti cha Udaktari wa Public Health (Honoris
Causa), kufuatia Shahada aliyotunukiwa na Chuo hicho mwaka 2010 kwa
Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza Sekta ya Afya nchini
leo Novermba 23, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa
Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko
wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel
Humba leo Novemba 23, Ikulu jijini Dar es salaam .
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu baada ya kupata
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha
Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health
Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba leo Novemba 23, Ikulu jijini
Dar es salaam.
K
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Wizara ya Afya na Mfuko wa
Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba
leo Novemba 23, Ikulu jijini Dar es salaam
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo Ijumaa Novemba 23, 2012 amepokea taarifa ya
maendeleo ya ujenzi wa Kampasi mbili za tiba ya afya vinavyojengwa
katika Chuo Kikuu cha Dodoma na Mloganzila huko Kisarawe, ambavyo pia
vitatumika kama hospitali hapa nchini.
Kwanza
Rais amepokea maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha
Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health
Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba .
Ujenzi wa kampasi hii umeshaanza na kufikia hatua ya juu na hospitali inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2015.
Kulingana
na Bw. Humba, maandalizi ya kufanikisha uanzishaji wa Chuo/ Hospitali
hiyo vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu wakiwemo Madaktari na
watumishi wengine wako nchini na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na
mafunzo mbalimbali.
Chuo
hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi
mahitaji ya Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa.
Rais
pia amepokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila
ambapo katika ujenzi na uanzishwaji wa Kampasi hizi zote, Rais Kikwete
amesimamia kuanzia hatua za awali.
Kampasi
ya Mloganzila ambayo ni sehemu ya Hospitali kuu ya Muhimbili inajengwa
kwenye eneo la ekari 3800 na itakua sehemu ya kutolea mafunzo kwa
wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya, lakini pia itakua sehemu ya
kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na ya kawaida nchini.
Ujenzi
wa Hospitali hii unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na
unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi.
Katika
hafla hiyo Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
Prof. Ephata Kaaya ametumia nafasi hiyo kumkabidhi Rais Kikwete Cheti
cha Udaktari wa Public Health (Honoris Causa), kufuatia Shahada
aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili
Disemba, 2010 kwa Kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kuendeleza
Sekta ya Afya nchini.
Akitoa
taarifa hiyo ya maendeleo kwa Rais Kikwete, Prof. Kaaya amesema tayari
wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya
Mloganzila wameshaanza mafunzo. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa
itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita
(600).
Rais
Kikwete amewapongeza wataalamu wote kwa juhudi zao na kuwa ahidi kuwa
lengo lake ni kuhakikisha nchi inaondokana na adha ya kupeleka wagonjwa
nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Rais
amesema moja ya lengo kubwa la serikali yake, ni kutoa kipaumbele
katika sekta ya Afya ili kuhaklikisha watanzania wanapata huduma bora,
kupanua mafunzo ya Afya na kuongeza wataalamu watakaoweza kutibu
magonjwa yote makubwa hapa hapa nchini.
Rais
amewaahidi watendaji wa Kampasi zote mbili kuwa atahakikisha ujenzi wa
huduma hizi muhimu kwa Umma haukwami kwa sababu ya ukosefu wa pesa
kwani ni jambo ambalo amedhamiria.
Imetolewa na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
23 Novemba, 2012.
0 comments:
Post a Comment