VITA ya maneno ndani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM), inazidi kupamba moto, baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu taifa, Hussein
Bashe kumtuhumu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe akisema ndiye anakivuruga chama hicho.
Mapambano
hayo yanatokea wakati wanaCCM wanakutana mjini Dodoma
kwa siku tatu katika mkutano wake mkuu, ambao utachagua viongozi wa kitaifa
watakaokiongoza chama hicho pamoja na wajumbe wa Nec 10 kutoka Tanzania Bara na
wengine kumi kutoka Zanzibar .
Bashe
pia alimtuhumu Membe kuwa anawatumia vijana wawili ndani ya chama hicho
kusambaza vipeperushi vya kumhujumu mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya
Kikwete na kumsingizia yeye na wenzake.
Kauli
ya Bashe inakuja siku moja baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho
kutoka Mkoa wa Morogoro, Augustino Matefu kumtaja Bashe, Makamu Mwenyekiti wa
UVCCM taifa, Beno Malisa na kada wa chama hicho, Fredrick Lowassa, kuwa
wanahusika kutawanya vipeperushi hivyo.
Vipeperushi
hivyo, ambavyo vilitawanywa katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma vilikuwa na ujumbe unaosomeka: “CCM
inayumba, kwa pamoja tumpunguzie mzigo mheshimiwa Rais kwa kumvua
kofia moja ya uenyekiti, nina imani kwa pamoja tutashinda, piga kura ya hapana
kwake, CCM oyeeee.”
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mjini Dodoma ,
Bashe alikanusha taarifa hizo akisema kuwa hajawahi kufikiria kumpinga Rais Kikwete
na kwamba maneno hayo ni uzushi juu yake.
“Lazima niwaambie kuwa hayo ni makundi yanayotengenezwa na baadhi ya watu, ili kunichafulia jina langu. Mwaka jana nilisema kuwa nitakuja kumtaja mtu huyo na leo namtaja kuwa ni Benard Membe, ndiye anayenisakama kupitia vijana wake,” alisema Bashe.
Alisema kuwa Membe kupitia kwa vijana wawili aliowataja kuwa ni Makonda na Matefu, alianza kumsakama tangu Aprili mwaka uliopita baada ya yeye (Bashe), kuteuliwa na UVCCM kuongoza kamati ya kutafuta maoni ya kuihuisha jumuiya hiyo.
“Kwanza lazima Watanzania wafahamu kuwa, Membe
ni mwongo, asiyekuwa na msimamo wakati wote. Nilisema na leo nataka ujumbe
umfikie na tayari nimeandika barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kumjulisha hilo ,” alisema Bashe.
Pia alimtuhumu waziri huyo kuwa amekuwa akiishi kwa kubebwa wakati wote akitoa mfano kuwa, mwaka 2005 alibebwa na Rostam Aziz kwa kumpatia gari lililomwezesha kwenda kuomba kura za ubunge na akapata.
Bashe pia alimtuhumu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa ni mshirika wa Membe katika harakati hizo za kukichafua Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nyalandu
Hata hivyo, Nyalandu alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo jana, alisema: “Waongo sehemuyao ni
katika ziwa liwakalo moto kwa kibiriti.”
Membe
“Lazima niwaambie kuwa hayo ni makundi yanayotengenezwa na baadhi ya watu, ili kunichafulia jina langu. Mwaka jana nilisema kuwa nitakuja kumtaja mtu huyo na leo namtaja kuwa ni Benard Membe, ndiye anayenisakama kupitia vijana wake,” alisema Bashe.
Alisema kuwa Membe kupitia kwa vijana wawili aliowataja kuwa ni Makonda na Matefu, alianza kumsakama tangu Aprili mwaka uliopita baada ya yeye (Bashe), kuteuliwa na UVCCM kuongoza kamati ya kutafuta maoni ya kuihuisha jumuiya hiyo.
“
Pia alimtuhumu waziri huyo kuwa amekuwa akiishi kwa kubebwa wakati wote akitoa mfano kuwa, mwaka 2005 alibebwa na Rostam Aziz kwa kumpatia gari lililomwezesha kwenda kuomba kura za ubunge na akapata.
Bashe pia alimtuhumu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa ni mshirika wa Membe katika harakati hizo za kukichafua Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nyalandu
Hata hivyo, Nyalandu alipotakiwa kuzungumzia tuhuma hizo jana, alisema: “Waongo sehemu
Membe
Alhamisi
wiki hii, Membe alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa kuna kundi la watu
ndani ya chama hicho, linalofanya kampeni chafu dhidi yake, lakini akasema
kwamba hujuma hiyo haitafanikiwa, badala yake atashinda kwa kishindo katika
uchaguzi wa Nec.
''Nakubaliana kabisa kwamba ziko njama za kunihujumu, ambazo hata mimi nazijua. Lakini wabaya wangu hao, wanafanya jambo ambalo hawalijui,kama
wangejua wasingepoteza muda huo,'' alisema Membe.
''Nakubaliana kabisa kwamba ziko njama za kunihujumu, ambazo hata mimi nazijua. Lakini wabaya wangu hao, wanafanya jambo ambalo hawalijui,
Alijifananisha
na mwembe, ambao hutupiwa mawe wakati wote kuliko mchongoma wenye miiba aliosema
hauwezi kutupiwa mawe kwani hauna kitu cha kuchukua juu yake.
Wazee
wanena
Baraza la Wazee wa CCM, Wilaya ya Dodoma Mjini jana walipinga kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kutaka madaraka ya Mwenyekiti wa chama hicho taifa yatenganishwe.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mwenyekiti wa Barazahilo , Balozi Job Lusinde,
alisema kuwa siyo jambo la busara hata kidogo kutenganisha nafasi hizo.
Lusinde alisema kwamba ni vyema Rais akaachwa kuendelea na shughuli zake pamoja na kofia zote mbili kwa kuwa ndiyo msingi na kanuni za chama.
Nec Vijana
Kwa upande wao wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia kundi la vijana, walisema kuwa watamlinda kwa gharama yoyote Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete pamoja na kuhakikisha kuwa anapata kura zote za ‘ndiyo.’
Baraza la Wazee wa CCM, Wilaya ya Dodoma Mjini jana walipinga kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kutaka madaraka ya Mwenyekiti wa chama hicho taifa yatenganishwe.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Mwenyekiti wa Baraza
Lusinde alisema kwamba ni vyema Rais akaachwa kuendelea na shughuli zake pamoja na kofia zote mbili kwa kuwa ndiyo msingi na kanuni za chama.
Nec Vijana
Kwa upande wao wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kupitia kundi la vijana, walisema kuwa watamlinda kwa gharama yoyote Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete pamoja na kuhakikisha kuwa anapata kura zote za ‘ndiyo.’
Mbali
na hilo , vijana
hao walisema kuwa watafanya kila njia kumsaka mtu aliyetengeneza vipeperushi
hivyo vinavyosambazwa dhidi ya mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete.
Wajumbe hao saba kati ya kumi waliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi za CCM Mkoa waDodoma na kutoa tamko hilo , huku wakieleza kuwa
hawatalala hadi watakapoona mwenyekiti wao akiibuka na ushindi wa kishindo.
Wajumbe hao saba kati ya kumi waliitisha mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi za CCM Mkoa wa
“Sisi
ndiyo jeshi la chama. Itakuwa ni aibu kama
mwenyekiti wetu atakuwa akidhalilishwa kwa kupata kura chache, ilhali nasi
tupo. Lazima kuwaaibisha watu wa aina hiyo na kuwasaka popote walipo. Tunaomba
vijana wenzetu watuamini kuwa tuko Dodoma
kufanya kazi hiyo,” alisema Jery Silaa kwa niaba ya wenzake.
CCM
Kagera
Naye Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kagera, Hamimu Omary, amekanusha uvumi uliozagaa kuwa Mkoa wa Kagera ni mmoja ya mikoa inayounga mkono mkakati wa kumhujumu Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kagera, Hamimu Omary, amekanusha uvumi uliozagaa kuwa Mkoa wa Kagera ni mmoja ya mikoa inayounga mkono mkakati wa kumhujumu Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete.
chanzo cha habari:gazeti la mwananchi
0 comments:
Post a Comment