Zikicheza bila
wachezaji wake muhimu na mihimili, Uholanzi na Ujerumani zilimaliza dakika 90
kwa sare isiyo ya mabao ndani ya dimba la Amsterdam ArenA
TIMU ya taifa ya Ufaransa, imeendelea kuimarisha kiwango
chake dimbani ilichoonesha katika sare ya 0-0 dhidi ya Hispania hivi
karibuni, ambapo usiku wa kuamkia leo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya Italia, shukrani kwa bao la mtokea
benchi Bafetimbi Gomis.
Stephan El Shaarawy alifunga bao la uongozi kwa Italia
kipindi cha kwanza, lakini Mathieu Valbuena akaifungia Ufaransa bao la
kusawazisha, kabla ya Gomis kufunga la ushindi akimalizia krosi ya Patrice Evra
kipindi cha pili.
Mabao sita yalitinga nyavuni katika pambano la kuvutia
jijini Stockholm , katika pambano baina ya
wenyeji Sweden waliobebwa na
mabao ya Zlatan Ibrahimovic katika ushindi wa 4-2 dhidi ya kikosi cha England
chini ya kocha Roy Hodgson.
Mabao kutoka kwa Danny Welbeck na Steven Caulker yaliashiria
mwanzo mwema wa mechi ya kirafiki, lakini Ibrahimovic akaonesha namna alivyo
hatari kwa kufunga mara nne, ikiwamo ‘tik-tak’ maridadi mwishoni mwa pambano hilo kuipa ushindi mnono
nchini yake.
Zikicheza bila wachezaji wake muhimu na mihimili, Uholanzi
na Ujerumani zilimaliza dakika 90 kwa sare isiyo ya mabao ndani ya dimba la Amsterdam
ArenA.
Mesut Ozil, Mario Gomez na Bastian Schweinsteiger yalikuwa
miongoni mwa majina makubwa ya Ujerumani yaliyokosa mechi hiyo, kama ilivyokuwa kwa Robin van Persie na Wesley Sneijder
waliokosekana kwa upande wa Uholanzi.
MATOKEO YA MECHI NYINGINE
DUNIANI
NOVEMBA 15, 2012
NOVEMBA 14, 2012
Italia 1 – 2 Ufaransa
Jmahuri ya Ireland
0 – 1 Ugiriki
Uholanzi 0 - 0 Ujerumani
Uturuki 1 – 1 Denmark
0 comments:
Post a Comment