.

.
Monday, November 12, 2012

5:34 AM
Unajua kuwa Tanzania ina idadi kubwa zaidi ya watu wazima wanaokojoa vitandani kuliko kenya na hata Uganda?

Tanzania ina watu wazima vikojozi, laki 5 ! Kenya inafuata karibu kabisa kwa kuwa wanaume na wanawake laki laki 4.

Wanasayansi wanasema tatizo hilo la watu wazima kukojoa ni kubwa na linasumbua wengi lakini kwa sababu ni jambo la aibu wengi hawataki kulijadili.

Kuna mameneja wabunge na hata mawaziri ambao ni vikojozi

Takwimu zinasema kwamba katika kila watu wazima 100, mmoja wao ni kikojozi.

hivyo nchini ikiwa na idadi ya watu milioni 50 kama Tanzania, basi jua kuwa watu wazima laki 5, yaani watu nusu milioni wanaokojoa wakiwa usingizini.

Jee unajua kuwa nchini uingereza kuna chama cha vikojozi? Watu wazima wanaokojoa wakiwa usingizini mjini London wameanzisha chama kinachoitwa The Bladder And Bowel Foundation.

KWANINI

Lakini kwanini mtu mzima na heshima zake au msichana mrembo au na matatizo ya kukojoa kitandani?

Daktari Zaki Almallah , mtaalam wa vibofu vya mikojo anasema taiba ya watu wazima kuwa vikojozi inarithishwa, kama baba au babu alikuwa kikojozi basi kuna uwezekano wa asilimia 40 kwa mtoto au mjukuu kuwa kikojozi ukubwani.

Wataalam katika Hospitali ya Birmingham nchini Uingereza wanasema sababu nyengine ni kutokomaa kwa tezi pituitary gland inayopatikana ndani ya ubongo chini ya sikio.

tezi hii hutoa homoni yakje a chembe cheme zake wakati wa usiku hivyo kuzuia utengenezaji wa mikojo. hivyo tezi hiyo ya pituitary gland ikiwa dhaifu au haikukomaa basi chembe chembe hizo zitatuma ujumbe kuwa mikojo zaidi itengenezwe, hivyo basi mtu kuwa na baala ya kujikojolea akiwa amelala maana ni lazima zitoke.

Mtu kuwa na stress,au msongo kuna weza kumsababishia mtu matatizo ya ukojozi.

Mheshimiwa mmoja , mkuu fulani serikalini, afrika mashariki ni kikojozi, lakini anamshukuru mkewe kwa kumvumilia?

Wewe unaweza kumvumilia mkeo au mumeo akiwa kikojozi...?
chanzo:BBC


0 comments:

Post a Comment