Na Rashid Nchimbi wa Polisi Arusha
Watu
watatu kati ya watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa baada ya
kupigwa risasi na askari wa Jeshi la Polisi. Tukio hilo lilitokea jana
muda wa saa 3:45 asubuhi katika eneo la olmatejoo lililopo jijini
Arusha.
Akithibitisha
taarifa hizo ofisini kwake jana mchana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas alisema kwamba,
walipata taarifa toka kwa raia wema juu ya uwepo wa watu watano
waliokuwa wanatiliwa shaka katika eneo la olmatejoo.
Kamanda
Sabas aliongeza kwa kusema kuwa, mara baada ya kupata taarifa hiyo,
baadhi ya askari waliokwenda katika eneo hilo kwa nia ya kufanya
uchunguzi, lakini watu hao walishtuka na mmoja wao alichomoa bastola
kiunoni na kuanza kuwafyatulia risasi askari hao.
Kufuatia
hali hiyo askari hao waliamua kujibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi
watu watatu ambao walichukuliwa na kupelekwa hospitali huku wengine
wawili akiwemo aliyekuwa na bastola wakifanikiwa kukimbia. Wakiwa
njiani kwenda hospitali ya Mount Meru watu hao walifariki dunia.
“Mara
baada ya mapambano ya kurushiana risasi askari walifanikiwa kupata begi
la watu hao na baada ya kulipekua walikuta bunduki mbili; moja aina ya
Shortgun na nyingine aina ya Rifle yenye namba 08805 ambayo ilikuwa
imekatwa kitako pamoja na mtutu, risasi 16 za shortgun, kipande cha
chuma (mtalimbo) ambacho kinasadikiwa kutumika katika uvunjaji.”
Alifafanua Kamanda Sabas
Mbali
na orodha hiyo pia begi hilo lilikutwa na rungu, panga, tupa tatu za
kunololea, kofia mbili zinazotumika kuficha uso na sare za Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo ni kofia moja, suruali moja na
T-shirt moja. Pia askari hao walifakiwa kupata kitambulisho cha kura na
kitambulisho cha Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Dodoma pamoja na
leseni ya udereva ambavyo wamiliki wake bado hawajapatikana.
Mpaka
hivi sasa majina ya watu hao ambao ni wanaume bado hayajajulikana na
Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea na juhudi za kutafuta majina
yao. Pia Jeshi hilo linaendelea kuwasaka watu wengine wawili ambao
walifanikiwa kukimbia. Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika
hospitali ya Mount Meru.
Kamishna
huyo Msaidizi wa Polisi alimalizia kwa kutoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa
Arusha kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa
za uhalifu na wahalifu. Pia alionya kwa kusema kwamba, watu
wanaofikiria kufanya uhalifu katika kipindi cha kuelekea mwisho wa
Mwaka waondoe kabisa mawazo hayo kwani Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
lipo imara kila kona.
0 comments:
Post a Comment