Meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo anayedaiwa kukataliwa na baadhi ya madiwani wa chadema |
Baadhi ya madiwani wa jiji la
Arusha wakiwemo madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
wameingia katika kashfa nzito kwenye sherehe za uzinduzi wa jiji hilo
zilizofanyika hivi karibuni na kuhudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete kama mgeni
rasmi.
Kuingia katika kashfa hiyo kunatokana na msimamo uliowekwa na chama hicho kwa madiwani wake kutohudhuria vikao vyovyote wala shughuli yoyote ya jiji hilo inayoongozwa na mstahiki meya wa jiji hilo Gaudance Lyimo ambao wao wanampinga na kutomtambua kwa kuwa hakupatikana kihalali.
Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu mkurugenzi wa jiji hilo Omar Mkombole katika kutolea ufafanuzi wa tuhuma hizo zilizoandikwa na gazeti moja la wiki alithibitisha kushiriki kwa madiwani hao wakishirikiana na madiwani wa vyama vingine kikiwemo CCM na TLP.
Mkombole alisema madiwani hao walishiriki na kutoa michango
"mimi kama mkurugenzi ni kiongozi wa kila diwani na ninapaswa kutoa ushirikiano kwake, kama wana tofauti zao ambazo nazifahamu kati
Kwa mujibu wa taarifa ya jiji hilo iliyotolewa na afisa habari wake Nteghenjwa Hossea ilitaja madiwani wa Chadema waliohudhuria vikao vya maandalizi ya shughuli hiyo kuwa ni mwenyekiti wa madiwani wa Chadema Issaya Doita wa kata ya Ngarenaro,Ephata Nanyaro(Levolosi),Viola Lazaro na Sabina Francis(wote wa viti maalumu) ikiwa ni pamoja na diwani wa chama cha TLP Michael Kivuyo wa kata ya Sokon One.
Mkurugenzi huyo alipoulizwa tangu lini madiwani hao wa Chadema walianza kushiriki vikao vya baraza la madiwani au walishiriki kwakua shughuli hiyo ilikua na maslahi alisema ni muda mrefu sasa madiwani hao wamekuwa wakiingia na kusaini posho kisha kutoka nje ambapo ushahidi wa mikanda ya video waliyo rekodi na sahihi katika vitabu vya mahudhurio wanazo.
Alifafanua kuwa matumizi hayo yalitumika kutokana na fedha walizopata kutoka mamlaka ya maji safi na maji taka jiji la Arusha(AUWSA)kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 18 kwa ajili ya kukarabati mnara,kampuni mbili za ujenzi wa barabara za ndani ya jiji zilizotoa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 12 na nyingine ikitoa milioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa jiwe la msingi na mapambo yote, huku wao kama jiji wakichangia shilingi milioni 89,533,000.50 kugharamia matumizi mengineyo ikiwemo chakula.
Alitaja matumizi mengi yaliyofanyika katika fedha hizo ni kulipa wasanii wa kundi la Komedi kiasi cha shilingi milioni 12 ,malipo ya msanii wa muziki wa kizazi kipya shilingi milioni 10,ununuzi wa njiwa wapatao 10 kwa shilingi 12,000 na sio njiwa 100 kama ilivyodaiwa kiasi cha shilingi 229,000 ikiwa ni gharama za kuwahifadhi njiwa hao pamoja na chakula na siyo shilingi 1,620,000 kama ilivyodaiwa na gazeti hilo la wiki.
Matumizi mengine ni kulipa kikundi cha JKT kiasi cha shilingi 1,000,000 na siyo shilingi 1,500,000 kama ilivyodaiwa pia alieleza kuwa kiasi cha shilingi 2,475,000 zilizotumika kununua zulia jekundu na kudai kuwa si kweli kwani zulia lilikodiwa katika hoteli ya Kibo Palace kwa shilingi 500,000.
Hata hivyo Mkombole alidai kuwa hakuna kikundi kilicholipwa fedha na kuacha kutokea kama ilivyodaiwa katika habari iliyoandikwa na gazeti hilo pia kwakua kikundi cha Kimasai kinachodaiwa kulipwa shilingi 1,050,000 kilitumbuiza katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA mara Rais alipowasili uwanjani hapo na Diamond kuzunguka mtaani kuhamasisha watu kuja uwanjani ambayo -->
Nembo ya jiji la Arusha |
Akizungumzia
suala mmoja wa madiwani hao wa CHADEMA Ephata Nanyaro wa kata ya Levolosi alikiri kushiriki
vikao hivyo kwa madai kuwa wamekuwa wakifanya hivyo kwa kuchagua baadhi ya
vikao na si vikao vyote vinavyofanyika wanashiriki.
Alisema hata yeye akiwa katika vikao hivyo alibaini kuwepo kwa ufisadi kutokana na matumizi ya fedha za maandalizi ya sherehe hiyo ila alishindwa kujitoa kutokana na kulazimishwa kushiriki katika kamati ya chakula cha Rais.
Alisema lengo lake la kushiriki ni kutokana na utaalamu alio nao katika sekta ya utalii kwa zaidi ya miaka kumi ili aweze kutoa mchango wake katika sherehe hiyo muhimu.
Alipoulizwa kuhusu kushiriki katika tuhuma za ulaji wa fedha katika sherehe hiyo Nanyaro alisema yeye hatambuikama kuna
ufisadi huo kwakua yeye katika kamati yake ya chakula alipangiwa kiasi cha
shilingi milioni 15 kwaajili ya kuwalisha wageni 200 fedha ambayo ilikua ni
nyingi kuliko mahitaji kwakua ilikua kila mgeni atumie kiasi cha shilingi
75,000.
Alisema mara baada ya kuonahilo
alijitahidi kushawishi kupunguzwa kwa kiasi hicho cha fedha ambapo iliwezekana
kupungua hadi kufikia kiasi cha shilingi milioni 7 na nyingine alizirejesha
katika kamati kuu ya maandalizi ambayo hajui ilitumika vipi.
Hata hivyo Nanyaro alipohojiwa kuhusu kususia vikao vinavyohusu maslahi ya wananchi wanaowawakilisha na kushiriki vikao hivyo vilivyokua na posho ya shilingi 100,000 ni sawa na kufanya kazi za maslahi yao Nanyaro alijibu kuwa kwasasa wanapanga mpango mpya wa kumkataa meya huyo ili awe anaondoka yeye katika vikao na kuacha kutoka wao na kususia viako ili kutetea maslahi ya wananchi wao.
-->Uzinduzi
huo wa jiji ulifanyika mnamo Novemba 1 mwaka huu kufuatia iliyokua halmashauri
ya manispaa ya Arusha kupandishwa hadhi ya jiji na wizara ya tawala za mikoa na
Alisema hata yeye akiwa katika vikao hivyo alibaini kuwepo kwa ufisadi kutokana na matumizi ya fedha za maandalizi ya sherehe hiyo ila alishindwa kujitoa kutokana na kulazimishwa kushiriki katika kamati ya chakula cha Rais.
Alisema lengo lake la kushiriki ni kutokana na utaalamu alio nao katika sekta ya utalii kwa zaidi ya miaka kumi ili aweze kutoa mchango wake katika sherehe hiyo muhimu.
Alipoulizwa kuhusu kushiriki katika tuhuma za ulaji wa fedha katika sherehe hiyo Nanyaro alisema yeye hatambui
Alisema mara baada ya kuona
Hata hivyo Nanyaro alipohojiwa kuhusu kususia vikao vinavyohusu maslahi ya wananchi wanaowawakilisha na kushiriki vikao hivyo vilivyokua na posho ya shilingi 100,000 ni sawa na kufanya kazi za maslahi yao Nanyaro alijibu kuwa kwasasa wanapanga mpango mpya wa kumkataa meya huyo ili awe anaondoka yeye katika vikao na kuacha kutoka wao na kususia viako ili kutetea maslahi ya wananchi wao.
0 comments:
Post a Comment