Mkuu wa usalama barabarani mkoani Arusha (RTO), Harison Mwakyoma akizungumzia ajali za barabara ofini kwake |
Watu 152 wamefariki dunia na
wengine 798 wamejeruhiwa mkoani Arusha
kufuatia ajali mbalimbali zilizotokea
mkoani hapa kuanzia mwezi January hadi
September mwaka huu.
Akizungumza na Bertha blog mkuu wa usalama barabarani
mkoani Arusha, kamanda Harison mwakyoma alisema kuwa vifo hivyo vimetokana na
ajali 1637 vilivyotokea kuanzia mwenzi wa kwanza mwaka huu hadi wa tisa ambapo
kati ya ajali hizo 129 ndizo zilizosababisha vifo hivyo vya watu 152.
Aidha alisema kuwa mbali na
vifo hivyo pia watu 1082 wamejeruhiwa kwenye ajali 798 zilizotokea kuanzia
mwezi wa kwanza hadi wa tisa mwaka huu ambapo alisema kuwa kwa sasa ajali
zimepungua kulinganishwa na ajali za mwaka jana.
Akitaja watu waliopoteza
maisha mwaka jana alisema watu 198 walikufa katika ajali 164 huku watu 1305
wakijeruhiwa katika ajali 835.
Kamanda Mwakyoma alisema kuwa
ajali kwa mwaka huu zimepungua kwa asilimia 84 ambapo jitihada hizo
zimefanikiwa kutokana na mafunzo wanayoyatoa kwa sasa hasa kwa madereva wa
bodaboda pamoja na opereshen ya kuwakamata wenye makosa ambao ndio wanaoongoza
kwa kusababisha ajali za mara kwa mara pamoja na vifo vya kila siku.
Alisema kuwa kabla ya mafunzo
kila siku walikuwa wakipata taarifa za ajali za bodaboda 2-3 lakini kwa sasa
inapita siku 3-4 hawana taarifa yoyote ya ajali za barabarani hali ambayo ni
mafanikio kwa jeshi la polisi kuwalinda wananchi na mali zao.
Mwakyoma aliongeza kuwa hadi
sasa wamekwisha toa mafunzo kwa madereva zaidi ya 1000 wa bodaboda kuwawezesha
kujua sheria, kanuni na taratibu za udereva hasa akiwa barabarani ambapo pia
amewataka madereva hao kuhakikisha kuwa kila dereva anakuwa na kofia ngumu
mbili(yaani element) kwa ajili ya dereva na mteja.
Sambamba na hilo kamanda Mwakyoma ameitaka jamii kuwa na
mtazamo chanya wa kusaidiana katika kupunguza vifo kwa kutopanda vyombo vya
moto kwa madereva wasio na mafunzo wala lesseni pamoja na kuhakikisha anapanda
piki piki ambayo dereva atampa element ya kuvaa ambayo itasaidia ajali itokeapo
kutokuumia au kufa.
0 comments:
Post a Comment