MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania, imekataa
kuifuta rufaa iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbles Lema (CHADEMA) kwa maelezo kuwa upungufu uliyopo kwenye nakala
ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, iliyotengua ubunge wake,
hauwezi kuwa sababu.
Lema alikata rufaa mahakamani hapo, akipinga hukumu iliyotolewa
Aprili 5 mwaka huu, na Jaji Gabriel Rwakibarila wa Mahakama Kuu Kanda
ya Arusha.
Uamuzi huo mdogo ulitolewa jana katika Mahakama ya Rufani jijini
Dar es Salaam na Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Zahara Maruma, huku
mamia ya wafuasi wa Lema wakiwa wamefurika kujua hatima yake.
Maruma alisoma uamuzi huo kwa niaba ya jopo la majaji wanaosikiliza
rufaa hiyo, Natalia Kimaro, Salum Massati wakiongozwa na Jaji Mkuu
Othman Chande.
Uamuzi huo unaotokana na pingamizi la awali lilowasilishwa na
wajibu rufaa ambao ni wananchama wa CCM wa la Arusha Mjini wanaotetewa
na Medest Akida na Alute Mughwai, dhidi ya Lema na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Arusha mjini na Mwanasheria
Mkuu wa Serikali anayewakilishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Timon
Vitalis.
Lema katika rufaa hiyo anawakilishwa na Method Kimomogoro na Tundu
Lissu ambao jana hawakuwepo mahakamani, ambapo wakili Edson Mbogoro
aliwawakilisha.
Jaji Chande alisema hivi karibuni wajibu rufaa waliwasilisha
pingamizi la awali ambapo waliwasilisha hoja tatu, akiiomba mahakama
hiyo iifute rufaa hiyo wakidai kuwa kikaza hukumu kilichotumiwa na Lema
kukata rufaa kilikuwa hakina mhuri wa mahakama wala haionyeshi hukumu
ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyotengua ubunge wake ilitolewa lini.
Kwamba walidai kuwa kikaza hukumu hakikuzingatia kanuni za Masijala
za Mahakama Kuu ya mwaka 2005 na kwamba kikaza hukumu hicho kilikuwa
kimekosekana maneno kama ‘hukumu hii imetolewa kwa mkono wangu’.
“Jopo langu limepitia hoja za pande mbili limefikia uamuzi wa
kukubaliana na hoja ya kwanza kuwa ni kweli kikaza hukumu kilichotumiwa
na Lema kukata rufaa kilikuwa na dosari hizo za kutokuwa na mhuri wa
tarehe, na tatizo hilo halikusababishwa na Lema ni watendaji wa
mahakama waliyoaanda kikakaza hukumu hiyo.
“Kwa sababu hiyo, mahakama hii imekataa ombi la wajibu rufaa
lililotaka mahakama hii ifute rufaa iliyokatwa na Lema kwa sababu eti
kikataa rufaa hicho kilikuwa na upungu huo, licha ya kwamba ni kweli
mahakama hii inakiri kuwepo kwa upungufu huo lakini hauwezi kufanya
mahakama hii iifute rufaa ya Lema,” alisema.
Alisema mahakama hiyo imempatia Lema muda wa siku 14 kuanzia jana
awasilishe upya rufaa yake ambayo atakuwa ameifanyia marekebisho
yatakayoonesha mhuri na tarehe ya kutolewa kwa hukumu ya Mahakama Kuu
Kanda ya Arusha.
Aidha, Jaji Chande alisema jopo lake limetupilia mbali hoja mbili
za wajibu makada wa CCM, zilizodai kikaza hukumu hakikuzingatia kanuni
za masijala ya Mahakama Kuu ya mwaka 2005 na kwamba kilikosa maneno;
‘hukumu imetolewa kwa mkono wangu,’ akisema hoja hizo hazina mantiki
kisheria.
Uamuzi huu ni wa pingamizi la awali na hausiani na rufaa iliyokatwa
na Lema mahakamani hapo kwani rufaa hiyo bado haijaanza kusikilizwa.
Oktoba 2 mwaka huu, pingamizi hilo la awali lilianza kusikilizwa
mjini Arusha ambapo wakili Kimomogoro alidai kuwa Jaji Gabriel
Rwakibarila wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, aliyetoa hukumu ya Lema,
jalada la kesi hiyo lilihamishiwa Dar es Salaam, hivyo hakukuwa na muda
wa kupitia hukumu na hati ya kukazia hukumu.
“Waheshimiwa majaji wa Mahakama ya Rufaa, wakili mwenzetu, Mughwai,
ametueleza hapa aliomba mara mbili tofauti apewe tuzo hiyo ikiwa
imesahihishwa, lakini hakupatiwa majibu, katika mazingira hayo
alitegemea sisi tungeipata vipi?” alihoji.
Baada ya uamuzi huo kutolewa jana, Lema alizungumza na wafuasi wake
nje ya mahakama hiyo, akisema anawashukuru wana-CHADEMA wa Dar es
Salaam kujitokeza kwa wingi kumfariji ambapo kwa sasa inayo imani na mahakama na siku si nyingi kesi yake itakwisha na ana uhakika wa kushinda kama haki itatendeka na kurudi bungeni kuwatetea wananchi wake.
0 comments:
Post a Comment