Na Shehe Semtawa
MILIONI sita zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya
mtoto Selemani Said (1), ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa
huku ukiwa nje ya tumbo lake imeleezwa.
Akizungumza na wandishi wa habari Katika Ukumbi wa
Idara ya Habari (Maelezo),jijini Dar es Salaam leo, mama wa mtoto huyo,
Veronika Laurent ambaye ni Mkazi wa Bunju, alisema mtoto huyo alizaliwa huku
akiwa na sehemu ya kutolea haja kubwa lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa
ikitokea mdomoni.
Alisema msaada wa fedha hizo utasaidia katika
kumfanyia operesheni mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi akiwa katika mateso
makubwa.
Veronika alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye
huyo wanaishi maisha ya kubahatisha baada ya baba wa mtotohuyo kuitelekeza
familia hiyo kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.
“Mimi ni nachoomba ni msaada wa fedha ili niweze
kumpeleka kwenye matibabu kwani sina msaada wowote,ukichukulia wazazi wangu
kufariki na hivi sasa naishi kwenye nyumba ya
mwenyekiti wa Mtaa wa Bunju wilayani Kinondoni jijini baada ya kushindwa
kupangisha chumba kwani sina kazi yeyote”alisema.
Aidha, alisema hadi utumbo wa mtoto huyo kutoka nje,
ni baada ya kufanyiwa operesheni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo
hata alipompeleka tena kwa ajili ya matibabu alikosa ushirikiano kutoka kwa
madaktari na wahudumu wengine.
Alisema kwa yeyote ambaye yuko tayari kumsaidia
anaweza wasiliana naye kwa kupiga simu namba o715 83 77 00, na namba ya
mwenyekiti huyo wa mtaa 0656780236.
Veronika ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro eneo la
Kijiji cha Uru,Moshi ambye alimzaa mtoto huyo na mwanamme aliyemtaja kwa jina
la Abdalah Said, kabilake makonde mfanyabiashara wa viatu Ubungo.
0 comments:
Post a Comment