Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wa Tanzania Bernard
Membe, amefanya mazungumzo na mabalozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya
waliopo mjini Dar es Salaam ili kuelezea pamoja na mambo mengine
mgogoro huo wa mpaka wa ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo
hayo na mabalozi wa EU, waziri Membe amesema, hivi sasa wanatarajia
kuongea na wenzao wa Malawi akiwemo rais Joyce Banda ili kuona
uwezekano wa kupeleka suala hilo katika Mahakama ya Kmataifa ya Sheria.
Kwa muda mrefu yamekuwapo mazungumzo kuhusu mgogoro wa mpaka huo na kupanuka kwa mgogoro huo hivi sasa kumechochewa na dalili za kuwapo kwa kiasi kikubwa cha gesi na mafuta katika ziwa hilo na hatua ya Malawi kuingia mkataba na kampuni moja ya uingereza ya kutafuta mafuta.

Waziri Membe amesema kabla ya kupeleka suala hilo la mgogoro wa mpaka
wa ziwa Nyasa katika mahakama hiyo ya kimataifa, timu ya wataalam wa
nyaraka kutoka Tanzania inakusudia kwenda Umoja wa Afrika, Uingereza na
Ujerumani kwa ajili ya kupata nyaraka muhimu juu ya suala hilo.
Katika mkutano huo na mabalozi wa EU waziri Membe pia alizungumzia vurugu za kidini zilizotokea hivi karibuni nchini Tanznaia na kueleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa ili kuweka uvumilivu wa kidini miongoni mwa watanzania.

Amesema Rais Kikwete pamoja na viongozi wengine kwa nyakati tofauti
wamekuwa wakikutana na viongozi wa makundi mbalimbali ya dini kuona
namna ya kudumisha uvumilivu wa kidini na uhuru wa kuabudu.
Waziri Membe pia alizungumzia suala la amani katika DRC Kongo kuhusu uamuzi wa nchi za SADC na nchi za maziwa makuu juu ya kupeleka majeshi nchini humo na msimamo wa serikali ya Tanzania juu ya hatua hiyo.

0 comments:
Post a Comment