UZINDUZI wa Jiji la Arusha uliofanyika wiki
Ijumaa iliyopita (Oktoba 2,2012) umekomba hazina ya Jiji
Jiji hilo lilizinduliwa na Rais Jakaya
Kikwete katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya
Sheikh Amri Abeid na kuhudhuirwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, kimataifa
na wananchi wa Arusha.
Hata hivyo, pamoja na sherehe hizo kufana,
tayari kuna taarifa za tuhuma kuwa sherehe hizo ziligubikwa na matumizi makubwa
ya fedha za Halmashauri ya Jiji
Katika mchanganuo wa awali ambao tumefanikiwa
kuuona
Dokezo
“Lengo la kuandika barua hii ni kuonyesha
hali halisi ya gharama tofauti na makisio yaliyopitishwa na kikao cha Kamati ya
Fedha cha tarehe 23/10/2012,” lilisomeka dokezo
Habari zilizotufikia baada ya sherehe hizo za
uzinduzi wa Jiji la Arusha, zinabanisha kwamba kiasi cha fedha hizo Sh milioni
100 zilizombwa katika dokezo hilo la Mweka Hazina, kilipunguzwa hadi kufikia
zaidi ya milioni 95, kabla ya Kamati ya Fedha kukutana tena, huku sehemu kubwa
ya fedha hizo ikiwa tayari matumizi yake yamefanywa na Mweka Hazina huyo pamoja
na watumishi wengine wa Idara ya Fedha.
Kwa mujibu wa mchanganuo uliopo, fedha ambazo
malipo yake yamezua utata katika dokezo hilo, yamehusu malipo kwa kikundi cha
wasanii maarufu cha Orijino Komedi kutoka jijini Dar es Salaam, ambacho
kinadaiwa kulipwa Sh milioni 12.0.
Malipo ya kiasi hicho cha fedha yalizua utata
mkubwa hata katika kikao cha Baraza la Madiwani ambapo
awali ilidaiwa kuwa wasanii hao walikubalina na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela, kulipwa kiasi cha Sh milioni 5.0 kwa shughuli ya kutoa burudani katika sherehe hizo.
“Katika hali ya kushangaza, Mweka Hazina
alilipa milioni saba zaidi tofauti na makubaliano ya awali na mkuu wa wilaya,
kwamba wasanii hao wangelipwa Shilingi milioni tano tu,” kinaeleza chanzo chetu
cha habari hizi.
Kibaya zaidi, chanzo hicho kinasema wasanii
hao wachekeshaji wa Orijino Komedi hawakupata nafasi ya kufanya onyesho lao,
zaidi tu ya kiongozi wao, Masanja, kupewa muda usiozidi dakika tatu kuwasalimia
wananchi waliohudhuria.
Hata hivyo juhudi za kumpata Mkuu wa Wilaya, John
Mongela, kuhusu taarifa hiyo ili kupata ufafanuzi zaidi hazikuweza kufanikiwa
hadi tunakwenda mitamboni.
Utata mwingine wa matumizi ya fedha,
unapatikana katika malipo ya msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond, ambaye
anadaiwa kulipwa Sh milioni 10.
Taarifa zaidi zinadai kuwa hatua ya kuwaalika
wasanii hao ilifikiwa kwa lengo la kuwavutia wananchi kuhudhuria sherehe hizo,
na hasa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa sababu za kisiasa. Inaelezwa kwamba
mji wa Arusha ni ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivyo
watu wengi wangepuuza sherehe hizo.
Mchanganuo huo umezidi kubainisha kuwa kiasi
cha Sh 26,000,000 kilitumika kutengeneza fulana 3,000 wakati Sh 2,475,000
zilitumika kununua zulia jekundu ambalo mgeni rasmi angepita juu yake. Aidha,
Sh 1,620,000 zinadaiwa kutumika kununulia njiwa 100 waliorushwa juu wakati wa
uzinduzi huo, ikiwa ni sawa na wastani wa Sh 16,200 kwa kila njiwa.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini
kwamba bei ya soko kwa njiwa moja ni kati ya Sh 2,500 na 3,000. Wachambuzi wa
mambo wanasema bei iliyotumika kunulia njiwa hao, ya kiasi cha 16,000 kwa njiwa
moja ni kubwa kuliko hata ya kuku wa kienyeji ambayo bei ya soko ni kati ya Sh
10,000 na 13,000.
Fedha nyingine zinazodaiwa kutumika vibaya ni
pamoja na Sh 1,050,000 zilizolipwa kwa kikundi cha ngoma za Kimasai ambacho
hata hivyo hakikutokea na wala hakikutumbuiza, pamoja na malipo ya Sh 1,500,000
kwa kikundi cha sanaa cha JKT Oljoro, ambacho nacho pia hakikupata nafasi ya
kutumbuiza.
Utata mwingine ni malipo ya Sh 2,475,000
zinazodaiwa kununulia zulia jekundu. Hadi sasa, haijaweza kuwekwa wazi kama
zulia
Matumizi mengine yanayozua utata, ni malipo
ya kukodisha Horn Speaker System kwa gharama ya Sh 1,000,000, uandaji wa ratiba
ya sherehe za uzinduzi wa Jiji la Arusha Sh 1,200,000 na uandaaji na usambazaji
wa barua za mialiko Sh 1,526,000.
Habari kutoka vyanzo vyetu vya kuaminika
zinasema kwamba baada ya baadhi ya madiwani wa kambi ya upinzani kuanza kuhoji
matumizi hayo, sasa maofisa wa halmashauri waliohusika na matumizi hayo
wanahaha kuweka hesabu sawa kwa kugushi hati za malipo kabla ya taarifa za
ufujaji huo wa fedha kuvifikia vyombo vya dola.
“Kwa jumla hali ni tete ndani ya Manispaa (ya
Arusha). Tayari kuna maofisa wameanza kuwa matumbo joto wakihofu kuwa suala
hilo linaweza kushikiwa bango na watendaji wa juu wa Serikali, hasa Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, ambaye ni kati ya viongozi wanaofahamika kwa
misimamo yao mikali kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma,” kinaeleza chanzo
chetu kutoka ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Akizungumzia utata wa matumizi hayo ya mamilioni
ya fedha, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Omar Mkombole alikanusha taarifa kuwa fedha
hizo zimetumika vibaya, huku akisisitiza kufanyika kwa uhakiki wa matumizi ya
fedha zilizotumika.
Anasema Mkombole: “Kwa sasa watu wa idara
fedha wana ‘consolidate’ matumizi ya fedha na taarifa kamili itapatikana baada
ya kesho (Jumanne) hivyo ni vizuri tusubiri, tuvute subira.”
Kwa uapande wake, Meya wa Jiji la Arusha,
Gaudance Lyimo, akizungumza kwa simu, alisema hana taarifa kuhusu matumizi ya
fedha kwa kuwa hakuwapo wakati wa kikao cha Kamati ya Fedha.
“Sifahamu chochote kuhusu mchanganuo wa
matumizi kwa kuwa kwa bahati mbaya nilikuwa nje ya ofisi kwa dharura hivyo
sijui maamuzi waliyofikia,” alisema Lyimo.
Diwani wa CHADEMA, Kata ya Levolosi, Ephata
Nanyaro, alisema wanapinga matumizi ya kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa
sherehe ya saa tatu tu wakati halmashauri ina mahitaji mengi ya kuwahudumia
wananchi.
“Walileta mchanganuo wao kwenye Baraza la
Madiwani na sisi tulikataa kwa kuwa tayari kuna malipo mengi yalishafanyika
tukawa tunawahoji tunajadili nini wakati malipo
Diwani huyo alielekeza lawama kwa Kamati ya
Fedha ya Baraza la Madiwani kwa kuridhia matumizi ya fedha hizo na kuongeza
kuwa watumishi wasio waaminifu wanapata mwanya wa kuiba fedha za umma kutokana
na udhaifu wa madiwani.
Jiji la Arusha lilizinduliwa wiki iliyopita
baada ya danadana za muda mrefu kutoka serikalini kutokana na sababu
mbalimbali, zikiwemo za kisiasa na uongozi wa iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa
ya Arusha kushindwa kufanikisha mahitaji muhimu yanayokidhi kulifanya kuwa
Jiji.
| |||||||
chanzo cha habari: gazeti la Raia mwema |
Home
»
»Unlabelled
» Fahamu mchanganuo wa gharama za uzinduzi wa jiji wenye ufujaji wa hali ya juu ya fedha za hazina la jiji hilo
Monday, November 12, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment