John Bocco 'Adebayor' akigombea mpira na beki wa Sudan |
Mashabiki Stars kwa raha zao |
Wachezaji Stars wakimpongeza Bocco baada ya kufunga bao la kwanza |
Benchi la Ufundi Stars, kutoka kushoto kocha Mkuu, Kim Poulsen, Msaidizi wake, Sylvester Marsh, Meneja, Leopold Tasso 'Mukebezi na kocha wa makipa Juma Pondamali |
Amir Maftah akimtoka beki wa Sudan |
Erasto Nyoni akitafuta mbonu za kumtoka beki wa Sudan |
Salum Abubakar akigombea mpira na kiungo wa Sudan |
Simon Msuva akigombea mpira na beki wa Sudan |
Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Sudan |
John Bocco aliingia nao mpira nyavuni kufunga bao la pili |
Wachezaji Stars wakimpongeza Bocco kushoto kwa kucheza sebene |
TIMU ya soka
ya taifa ya Tanzania Bara, imeanza vema kampeni zake za kuwania Kombe la
Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, baada ya kuichapa
mabao 2-0 Sudan katika mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Mandela,
Namboole, Kampala, Uganda.
Ushindi huo,
unaiweza Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika nafasi ya pili kwenye msimamo
wa Kundi B, nyuma ya Burundi inayoongoza kwa wastani wa mabao.
Hadi
mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yote yakipachikwa kimiani na
mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ aliyetumia vema krosi za
Mrisho Khalfan Ngassa.
Bocco
alifunga bao la kwanza Bocco aliiwahi vema krosi ya Ngassa aliyewatoka mabeki
wa Sudan wingi ya kushoto na kuitumbukiza kimiani dakika ya 14.
Adebayor wa
Chamazi aliwainua tena vitini mashabiki wa Tanzania dakika ya 28, akiunganisha
krosi ya Ngassa tena kutoka kule kule kushoto.
Kwa ujumla
Tanzania Bara walicheza vizuri kipindi cha kwanza, wakishambulia zaidi kupitia
pembeni, kulia Simon Msuva ambaye hakuwa na madhara sana na kushoto Ngassa
ambaye alikuwa mwiba mchungu haswa kwa Wasudan.
Pamoja na
Bara kutawala kipindi cha kwanza, lakini Wasudan walifanya mashambulizi kadhaa
ya kushitukiza na sifa zimuendee mlinda mlango Juma Kaseja, ambaye alioko
amichomo miwili ya hatari mno.
Kipindi cha
pili Stars, inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen iliendelea kutawala mchezo,
lakini safu ya ulinzi ya Sudan iligangamala.
Tanzania Bara; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir
Maftah, Shomari Kapombe, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba,
John Bocco, Mwinyi Kazimoto na Simon Msuva/Shaaban Nditi.
Sudan; Ebd Elrahman Ali, Moawia El Amin,
Sami Abdallah, Faris Abdallah, Hamoda Bashir/Farid Mohamed, Mohamed El Mortada,
Sadam Abutalib, Mohamed Mussa Idris, Modathir Mohamed, Adam Sayer/Osama El
Rashid na Mohamed Osman/Saed Siddig.
Katika
mchezo wa awali, Burundi walishinda mabao 5-1, mabao yake yakifungwa na Chris
Nduwarugira dakika ya 35 na 88, Yussuf Ndikumana dakika ya 41 na Suleiman
Ndikumana dakika ya 84 na 90, wakati la Somalia lilifungwa na Mohamed Jabril
kwa penalti dakika ya 55.
Matokeo hayo
yanalifanya Kundi B lizidi kuwa gumu, kwani Burundi inaongoza kwa pointi zake
tatu na mabao mengi, Tanzania ya pili kwa pointi tatu na mabao mawili- lakini
bado Sudan wanaweza kupata matokeo mazuri katika mechi zijazo.
STARS YAANZA KAZI KAMPALA LEO USIKU
John Bocco 'Adebayor' ataongoza safu ya ushambuliaji Stars leo? |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
TIMU ya
taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars leo inatarajiwa kuanza kampeni zake
za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker
Challenge leo itakapomenyana na Sudan kuanzia saa 12:00 jioni Uwanja wa
Mandela, Namboole mjini hapa.
Mchezo huo,
utatanguliwa na mchezo mwingine wa Kundi B kati ya Somalia na Burundi, kuanzia
saa 10:00 jioni kwenye Uwanja huo huo.
Kocha wa Kilimanjaro
Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesikitishwa na kutowasili kwa washambuliaji Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC).
“Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kwanza kwa
sababu hawajafika, lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na
wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani
TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi
karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,”
alisema.
Alisema
wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza
dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo
zitacheza leo pia.
Hata hivyo,
jana Kili Stars walilalamikia Uwanja mbovu wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya
Biashara, waliopelekwa kufanya mazoezi kujiandaa na mechi ya leo.
Ofisa Habari
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura aliwasilisha malalamiko
hayo kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rodgers Mulindwa
ambaye ameahidi kuyafanyia kazi.
“Tutalifanyia
kazi suala hilo, tutakuwa na kikao kesho (leo) litawasilishwa na litapatiwa
usumbufu, mwanzo huwa na matatizo, lakini mambo yatakuwa mazuri,”alisema
Mulindwa.
Hata hivyo,
inashangaza Stars kupelekwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya
Biashara, wakati kwenye mpango wa awali kabisa wa FUFA ilitakiwa kufanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Nakawa.
0 comments:
Post a Comment