Na Mwajuma Ernest-Karatu
Serikali imetakiwa kutoa
elimu ya sheria, kanuni na taratibu za umiliki wa ardhi kwa wananchi wake ili
kuweza kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la migogoro ya ardhi inayotokea mara
kwa mara.
Rai hiyo imetolewa na
mwanansheria wa kujitegemea Pascal hillu kwenye mdahalo wa umiliki wa ardhi uliofanyika jumatatu wilayani karatu
Bwana Pascal alisema kuwa
migogoro ya ardhi inayoendelea kwa sasa katika maeneo mbalimbali hapa nchini
inasababishwa na wananchi kutotambua sheria na kanuni na taratibu za umiliki wa
ardhi hivyo serikali imalize tatizo hilo
kwa kutoa elimu hiyo kwa wananchi wake.
Alisema kuwa pamoja na
mapungufu hayo pia serikali imekuwa ikiajiri watendeji katika sekta wasio na
elimu
ya sheria za ardhi hali
inayosababisha kutenda kazi kwa kuendekeza rushwa na kutoa maamuzi yasiyo ya
haki na kusababisha migogoro zaidi kwa wale wanaoonewa
Akitolea mfano alisema kuwa
rushwa imekuwa ikitawala sana
hasa katika kutoa hati miliki ya ardhi ambapo watendaji husika hasa maafisa
ardhi hudai rushwa la sivyo upatikanaji wa hati hiyo huwa ni ngumu na kuchukua
mda mrefu.
Kwa upande wake katibu
madahalo huo Best Ptrick aliiomba serikali kupitisha sheri ya kuweza kumshitaki
afisa ardhi yeye ka ma yeye kuliko sasa ambapo anayefanya kosa ni mtendaji
lakini serikali ndio hushitakiwa huku mtendeji akiendelea na utendaji mbovu
ikiwemo kula rushwa.
Mdahalo huo ulioandaliwa na
taasisi ya maendeleo isiyo ya kiserikali ya ijulikanayo kama
KDA (Karatu Development Association) liliwahusisha watu mbalimbali wakiwemo
wanafunzi, wanasiasa na viongozi wakiwemo wakiwemo wananchi.
Akizungumzia mdahalo huo
katibu huyo bwana Best alisema kuwa wameamua kuitisha mdahalo huo kuwasaidia
wananchi kuelewa sheria, na taratibu za umiliki wa ardhi baada ya kuona
migogoro ya mara kwa mara katika jamii ya kugombea ardhi.
0 comments:
Post a Comment