Kesi ya madai inayowakabili waliokuwa madiwani wa
chama cha demokrasia na maendeleo chadema leo imehairishwa katika mahakama kuu
ya kanda ya Arusha hadi hapo November 21 mwaka huu itakapo julikana
hatima yao
baada ya kushindwa kulipa fidia ya zaidi ya shilingi miolini 15 .
Kabla ya kuahirisha kesi hiyo hakimu mkazi mfawidhi
,Charles Magesa anayesikiliza kesi hiyo ,alisikiliza hoja za pande zote
mbili,ambapo wakili wa chadema, Method kimomogoro aliitaka mahakama
iwachukulie hatua kali wahusika kwa kushindwa kulipa fedha hizo
zilizoamuriwa na mahakama,April 10 mwaka huu.
Pia akimu kimomogoro aliiambia mahakama kwamba wadaiwa
hao wamekuwa wasumbufu kwa kutaja kiwango kidogo cha kulipa ambacho ni kinyume
na vipato vyao kwani katika mahesabu ya haraka inaonyesha kuwa kwa garama
walizotaja wanaweza kulipa watatumia muda wa zaidi ya miaka 10 hadi kumaliza
kumlipa mteja wake.
“muheshimiwa hakimu huoni kuwa kwa kila moja
walivyojieliza kulipa kiasi hicho mara shilingili 15,000 kwa mwezi na wengine
25,000 watatumia mda mrefu mno,watakuwa wanatania maakama maana kunaambao
wanawanavitega uchumi kibao huku wengine wakimiliki magari na wengine
wakimiliki magari kwanini wasiuze au kukodisha na kama tukiwasikiliza si
tutakuwa tunapotezea mda mahama “alisema kimomogoro
Kwa upande wa madiwani hao ambao ni Charles
mpanda,John bayo ,robern ngowi ,Rehema Mohamed pamoja na Estomy Malla mmoja wa
madiwani hao John Bayo akiongea mahakamani hapo alisema kwamba hawakatai kulipa
lakini watalipa kutokana na vipato vyao na kuiomba mahakama ikubali kukubali
kulipa viwango walivyovitaja.
Mara baada ya hoja za pande zote mbili kukamilika
hakimu Magesa alihairisha kesi hadi hapo November 21 (kesho kutwa)ambapo ndipo
maamuzi kamili yatatolewa.
Akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama method
kimomogoro alisema kuwa Awali mteja wake chadema alipeleka mahakamani madai ya
zaidi ya shilingi milini 2 9 lakini mahakama ilichambua na kuwataka walipwe
shilingi 15,116,500 huku akibainisha kuwa wao wanasubiri mahamuzi ya mahakama
apo kesho kutwa na iwapo wataamriwa walipwe watapokea .
“sheria ya mahakama inasema kuwa ukimpeleka mtu magereza
unatakiwa umlipie hela ya chakula sasa wakishindwa kulipa tupo tayari kuwalipia
chakula ili waende kusota magereza hadi pale watakapo lipa”alisema Kimomogoro
Aidha alibainisha kwamba iwapo mahakama itawahukumu
kifungo fedha za chakula watawalipia na kuzijumlishia kwenye deni la mteja
wake.
0 comments:
Post a Comment