Juma Kaseja |
KATIKA kuhakikisha ari ya wachezaji inarudi kama ilivyokuwa mwanzo, uongozi wa klabu ya Simba una mpango
wa kuipeleka timu nje ya nchi ili kuwapa muda wachezaji wa kusahau yaliyopita
na kujipanga vema kwa mzunguko wa pili.
Aidha, uongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, umemuomba radhi kipa na nahodha wake, Juma Kaseja kutokana na
kudhalilishwa na baadhi ya watu baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo
usioridhisha katika michezo yake ya mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema leo kwamba kudhalilishwa kwa
Kaseja si sahihi kwani anaweza kukofanya makosa ya kiufundi kama binadamu
mwingine, hivyo anahitaji ushauri wa kimawazo.
“Tuache kudhalilisha
wachezaji kwani kufanya hivyo si uungwana wa michezo hata kidogo…kila mtu
anafahamu kuna kushinda, kufungwa na kutoka sare, kama hatutaki kufungwa
tujiondoe wenye ligi,”alisema Rage
0 comments:
Post a Comment