Katibu Mkuu wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha Eliya Mbonea (kushoto), akisaini nyaraka za makabidhiano ya
vifaa mbalimbali vya ofisi kutoka kwa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC jana katika ofisi za chama hicho jijini Arusha.
Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa fedha na utawala wa UTPC, Jackson Uisso.
vifaa mbalimbali vya ofisi kutoka kwa umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini UTPC jana katika ofisi za chama hicho jijini Arusha.
Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa fedha na utawala wa UTPC, Jackson Uisso.
MUUNGANO wa Vyama vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC) uimeikabidhi Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 35.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa jana Ofisa Utawala na Fedha wa
UTPC Jackosn Uiso katika ofisi za Klabu ya APC jijini hapa na kushuhudiwa na viongozi
na baadhi ya wanachama.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Uiso
aliwahimiza viongozi kuhakikisha vinatumika kwa wanachama ikiwa ni pamoja na
kuingizia fedha Klabu.
“UTPC inawahimiza mtumie vifaa hivi kwa uangalifu, lakini
hakikisheni mnaweka utaratibu wa jinsi gani vitawaingizia fedha za Klabu badala
ya kuendelea kuvifungia,” alisema Uiso.
Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mashine ya
kudurufu, Televisheni ya Inchi 32, Kamera kubwa ya kisasa kwa ajili ya picha za
mnato, mashine ya Projector, Desk Kompyuta na Laptop.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu aliwashukuru
UTPC kwa kukabidhi vifaa hivyo na kuahidi kwamba vitatumika kwa uangalifu
mkubwa.
“Vifaa hivi ni vya thamani na tunaahidi kuvitumia kwa
uangalifu utakaoleta manufaa kwa Klabu na wanachama wake,” alisema Gwandu.
Naye Katibu Mkuu wa APC Eliya Mbonea kwa upande wake aliwashukuru
UTPC kwa kufanyia kazi mawazo ya viongozi wa Klabu nchini waliopendekeza
kutumiwa vifaa vinavyolingana na taaluma.
“Mapendekezo ya viongozi wa Klabu yamefanyiwa kazi, awali
tulikuwa tunaletewa kamera ndigo zinazowapa wakati mgumu waandishi kupiga picha
hususani viongozi wa kitaifa wanapokuja au tukio linapokuwa mbali,” alisema
Mbonea na kuongeza:
“Mfano hii Kamera ya picha za mnato kweli hapa sasa
hatuwezi kulalamika tena kwamba hatuna kamera ya kisasa kwani Kamera hii
unaweza kupiga picha ukiwa mahali popote,” alisema.
chanzo:libeneke la kaskazini blog
0 comments:
Post a Comment