Alex Mgongolwa, Mwenyekiti wa kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji ya TFF
Katika
kikao chake cha tarehe 3 Novemba 2012, Kamati ya Utendaji ya TFF ilipokea
taarifa ya mapendekezo ya marekebisho ya Katiba TFF kama
ifuatavyo:
Kuingiza
kipengele kinachohusu “Club Lincencing” kama
ilivyoagizwa na CAF katika waraka wake unaowataka wanachama wote wa CAF,
ikiwemo TFF, kuhakikisha kuwa kipengele hicho kinaingizwa katika katiba zao.
Kutokana
na ushauri na maagizo ya FIFA, TFF inatakiwa kuunda wa Kamati ya Rufaa ya
Uchanguzi (“Elections Appeals Committee”) na kuondokana na utaratibu tulionao
hivi sasa ambao Kamati ya Rufaa (“Appeals Committee”) inajigeuza na kuwa Kamati
ya Rufaa ya Uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi wa TFF.
Kuindoa
nafasi ya Makamu wa Pili wa TFF pamoja na kutamka kuwa Wawakilishi wa klabu za
Ligi Kuu katika Kamati ya Utendaji watachaguliwa moja kwa moja na klabu
zenyewe. Hii inatokana na azimio la Mkutano Mkuu uliopita la kuruhusu uundwaji
wa chombo huru cha kusimamia Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na
kupitishwa kwa Kanuni zinazokiongoza chombo hicho kama zilivyopendekezwa na
klabu za Ligi Kuu na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.
Baada ya
kutafakari mapendekezo hayo, Kamati ya Utendaji ya TFF iliamua kuwa:
Ipo haja
ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TFF kama
iliyopendekezwa.
Kwa vile
mapendekezo mawili kati ya matatu ya ya marekebisho ya Katiba yana uhusiano na
Uchaguzi Mkuu wa TFF, ipo haja ya marekebisho hayo kufanyika kabla ya
kutangazwa kwa Mkutano Mkuu wa TFF na kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa
TFF.
Aidha,
kwa vile TFF haina uwezo wa kuitisha mikutano mikuu miwili – Mkutano Mkuu
Maalum kwa ajili ya marekebisho ya Katiba ya TFF; na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi –
katika kipindi kifupi kijacho, marekebisho ya Katiba yafanywe kwa njia ya
Waraka (“Circular Resolution”).
Waraka
huo (“Circular Resolution”) uwe umeshatayarishwa na Sekretariati ikishirikiana
na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ifikapo tarehe 15 Novemba 2012 na ukabidhiwe
kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaowakilisha Kanda za TFF ambao
watahakikisha kuwa kila Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa Kanda husika anapata fursa ya kutoa ridhaa yake.
Zoezi la
kupata ridhaa ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu liwe limemalizika katika kipindi cha
siku 21.
Kikao kinachofuata
cha Kamati ya Utendaji kitafanyika Jumamosi tarehe 15 Desemba 2012 kwa
madhumuni ya kupokea taarifa ya zoezi hili na kufanya matayarisho ya Mkutano
Mkuu. Katiba ya TFF inaelekeza kuwa taarifa ya Mkutano Mkuu itolewe kwa
wanachama wake angalau siku 60 (“notice period”) kabla ya Mkutano. Hivyo Kamati
ya utendaji inatarajia kuwa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utafanyika Jumamosi na
Jumapili ya tarehe 16 na 17 na Februari 2013.
Kamati
ya Utendaji ya TFF inasisitiza kuwa utaratibu huu umeamuliwa kutokana na TFF
kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kutayarisha mikutano mikuu miwili katika
kipindi kifupi kijacho. Kinyume chake ni kuchelewa zaidi kufanyika kwa Mkutano
Mkuu, jambo ambalo hatuna budi kuliepuka.
Kamati
ya Utendaji ya TFF inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa jumla ili kufanikisha
zoezi hili na hatimaye kufanikisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TFF.
Wenu
Katika michezo,
Alex
Mgongolwa
Mwenyekiti
KAMATI
YA SHERIA, MAADILI NA HADHI ZA WACHEZAJI
0 comments:
Post a Comment