Baraza la mawaziri nchini Kenya linapendekeza mabadiliko makubwa kwa sheria za ndoa nchini humo .
Mswaada
wawaliowasilisha unapendekeza kuwa wanaume wanweza kuoa zaidi ya mke
mmoja na hata kuharamisha mahari ambapo familia ya mwanaume inalipa
mahari hiyo.
Pia
inataka kuhalalisha watu kuishi pamoja kama mume na mke bila ya ndoa
kwa kipindi cha miezi sita kama njia ya kulinda watoto na wanwake
wakati uhusiano huo unapovunjika.
Mapendekezo
hayo tayari yamezua hisia kali kutoka kwa jamii kwa ujumla. Aidha
mswaada huo, lazima uidhinishwe na bunge kabla ya kufanywa sheria.
Wengi
wa wanaoishi maisha kama hayo ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo
uhusianao kama huo unajulikana kama "come we stay" au njoo tuishi
pamoja kama mke na mume bila ya ndoa.
Wanafunzi
hujipata katika uhusiano kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati
wakisoma na punde baada ya kuhitimu , huvunja uhusiano ule.
Mara nyingi watu huishi pamoja bila ya kuoana kwa sababu za manufaa ya ule uhusiano
Wakati
mwingine hata hupata watoto wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja ,
na hapo ndipo mwanamue hutafuta njia za kutoroka ili kukwepa majukumu
yake.
Na hilo ndilo lengo la mswaada huu kulingana na baraza la mawaziri.
Linasema
linataka ikiwa utakuwa sheria iweze kulinda akina mama na watoto
kutokana na dhulma za nyumbani hususan wanaume wanaokwepa majukumu yao.
Mswaada
huu umevutia hisia mbali mbali, baadhi wakisema kuwa itakwenda kinyume
na tamaduni na desturi za jamii, hasa ikizingatiwa swala la mahari
ambalo mswaada huo unapendekeza kutupiliwa mbali.
Dini nyingi kama Uisilamu na hata wahindi wanakumbatia swala na mahari kwa sababu ni matakwa ya dini.
Ingawa
baraza la mawaziri limepitisha mswaada huo, inaweza tu kuwa sheria
ikiwa bunge litaipitisha. Ikiwa kweli rekodi ya bunge hili ndio itakuwa
kigezo cha kupitishwa kwa mswaada huu, bunge lenyewe lenye asilimia
hamsini ya wanaume, litatupilia mbali mswaada huo au kuupitisha baada
kufanya mabadiliko.
Wengi wa wanaoishi
maisha kama hayo ni wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo uhusiano kama huo
unajulikana kama "come we stay" au njoo tuishi pamoja kama mke na mume
bila ya ndoa.
Wanafunzi huishi katika uhusiano kama huo kwa hata miaka minne au zaidi wakati wakisoma na baada ya kusoma huachana.
Mara nyingi watu huishi pamoja bila ya kuoana kwa sababu za kujinufaisha kwa hali yoyote ile.
Wakati
mwingine hata hupata watoto wakati wa kipindi kile wanapoishi pamoja ,
na hapo ndipo mwanamume hutafuta njia za kutoroka ili kukwepa majukumu
yake.
Mswaada huu umvutia hisia mbali
mbali, baadhi wakisema kuwa itakwenda kinyume na tamaduni na desturi za
jamii, hasa ikizingatiwa swala la mahari ambalo mswaada huo
unapendekeza kutupiliwa mbali.
chanzo cha habari: BBC
0 comments:
Post a Comment