Na Elizabeth John
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ally Momba ‘Momba’ anajipanga kuwapa ‘Surprise’ mashabiki wake kupitia kibao chake kipya ambacho hajataka kukitaja jina kutokana na maharamia waliopo katika fani hiyo.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salam, Momba amesema mwishoni mwa mwezi Desemba ataachia ngoma hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri kutokana na vitu adimu ambavyo vipo ndani yake.
“Siunajua wabongo, jina siwezi nikalitaja saivi maana nikitaja tu wajanja wataliwahi muda ukifika nitasema tu, ila mawazo niliyotumia saivi ni vitu adimu sana hivyo naomba mashabiki wangu wajipange kisawasawa,” alisema Momba.
Momba amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hiyo ambayo anaamini itakua gumzo mtaani kutokana na ubora ulionao.
Mbali na kutoka na kibao hicho, Momba alishawahi kutamba na vibao vyake kama Mimi sio Sharobaro, Kabwela, Mdundiko na nyinginezo ambazo zilifanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na luninga.
..................XXX.......................XXX.......................XXX...........
NYOTA wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Salim Mohamed ‘Sam wa Ukweli’ kesho anazindua video ya wimbo wake
mpya unaokwenda kwa jina la ‘Samaki’ ambao unafanya vizurikatika vituo
mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto
jijini Dar es Salaam jana, Sam amesema wimbo huo umeshaanza kufanya vizuri na
anawaomba mashabiki wafike kwa wingi ili waweze kushuhudia kilichopo ndani ya
samaki.
“Uzinduki huo utafanyika
ndani ya Maisha Club, Jumapili ya keshokutwa naomba mashabiki wa kazi zangu
wadondoke kwa wingi kwani ni video ambayo ipo tafauti na kazi zangu naomba
wanipe sapoti ya kutosha,” alisema Sam.
Amesema anawaomba wadau wa
muziki waendelee kumpa sapoti katika kazi zake bado kuna vitu vingi ambavyo
amewaandalia.
Licha ya kutamba na kibao
hicho, Sam wa Ukweli alishawahi tamba na vibao vyake kama Lonely, Sina raha,
Hata kwetu wapo na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika
muziki wa bongo fleva.
................XXX..........................XXX.......................XXX.........
BAADA ya kukaa kimya kwa muda
mrefu, Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Stephen William ‘Steve RnB’
amewataka wapenzi wa muziki nchini kukipokea kibao chake kinachokwenda kwa jina
la ‘Radio’.
Akizungumzia kibao hicho
jijini Dar es Salaam, Steve amesema kibao hicho kaachia hivi karibuni na kwamba
yupo kwenye hatua za mwisho za uandaaji wa video ya kazi hiyo.
“Ukimya wangu umetokana na
kwamba sikuwepo nchini kwa muda mrefu nilikuwa ninaziara ndefu kama miezi sita
katika nchi za Ujerumani, Australia na Italy kwaajili shoo iliyoandaliwa na
Wajerumani ambayo ilikuwa inaitwa ‘Mama Afrika,” alisema Steve.
Amesema kwasasa ameanza kazi
rasmi na kwamba watanzania watarajie vitu vizuri kutoka kwake kutokana na
uzoefu alioupata katika nchi hizo.
Mbali na hayo, Steve
alimpongeza mshindi wa Epiq Bongo Star Search (EBSS) 2012, Walter Chilambo kwa
kuimba wimbo wake wa ‘One Love’ na kuutendea haki kitua ambacho kimemfanya
ajisikie kama msanii ambaye anauwezo mzuri wa kuandika mashairi.
“Kiukweli nilijisikia furaha
sana kwa msanii mchanga kuutendea haki wimbo huo, kitua ambacho wasanii wengi
wanashindwa kutokana na ugumu wa wimbo wenyewe, namkaribisha katika ‘game,”
alisema Steve RnB.
0 comments:
Post a Comment