Taarifa
hiyo imetolewa siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu
mjini Kampala, Uganda, kuwasihi wapiganaji waondoke Goma.
Msemaji
wa wapiganaji, Kasisi Jean-Marie Runiga, alisema wapiganaji wataondoka
Goma baada ya mazungumzo ya amani lakini siyo kabla.
Rais Joseph Kabila wa Congo alikutana na wawakilishi wa wapiganaji mjini Kampala Jumamosi.
Wakuu wa Uganda wanasema yamekuwapo mawasiliano baina ya pande hizo mbili.
...........xxx.....xxx........xxx.........
Rais ataka jina la nchi libadilishwe
Rais wa Mexico amewasilisha mswada kwa bunge la Congress kutaka jina rasmi la nchi hiyo kubadilishwa.
Jina la sasa la jimbo la Mexico lilianza kutumiwa mwaka 1924 baada ya kupata uhuru kutoka Uhispania .
Hata hivyo halijakuwa likitumiwa na rais Felipe Calderon anataka libadilishwe na kuwa Mexico tu.
Ripoti
zinaonyesha kuwa Bwana Calderon alipendekeza kwa mara ya kwanza jina
hilo kubadilishwa mwaka 2003 lakini mswada huo haukupitishwa kwa kura.
......xxx....xxx....xx
Mabomu yaripuliwa kambini Kaduna
Jeshi
la Nigeria linasema kuwa mabomu yaliyotegwa kwenye magari mawili
yameripuliwa ndani ya kambi ya karibu na mji wa Kaduna, kaskazini mwa
nchi.
Watu kama 11 waliuwawa na 30 kujeruhiwa.
Mshambuliaji wa kwanza alikuwa kwenye basi lilojaa mabomu na aligonga kanisa wakati ibada ya Jumapili ikimalizika.
Dakika 10 baadae gari lilotegwa bomu liliripuka nje ya kanisa.
Jeshi la Nigeria limelaumu kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi alisema mashambulio hayo ndani ya kambi ilioko Jaji, yatia aibu.
Boko Haram inapigana kuipindua serikali ya Nigeria, ili kuweka sheria kali za Kiislamu.
chanzo na bbc
0 comments:
Post a Comment