Mkuu
wa majeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi
huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi
ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo.
Ripoti
moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa
kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu na makundi
ya waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali
ya Rais Kabila imemfuta kazi mkuu huyo wa majeshi, siku chache baada ya
waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi
hao mpia wameutekja mji wa Sake, lakini msemaji wa serikali Lambert
Mende, amesema wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuumboa tena mji huo
mdogo.
Waasi hao ambao wanaaminika kuungwa
mkono na serikali za Rwanda na Uganda, wametishia kuendeleza mapigano
hayo hadi mji mkuu wa Kinshasa, ikiwa rais Joseph Kabila hatabuli
kuanzisha mazungumzo ya amani.
Mazungumzo ya Amani
Uganda
inaandaa mkutano wa marais wa Rwanda na Uganda hii leo na kuna ripoti
kuwa baadhi ya viongozi wa kundi hilo la waasi wa M23 wamesafiri mjini
Kampala kushiriki katika mazungumzo hayo.
Ripoti
iliyoandikiwa Umoja wa Mataifa na kundi moja wa wataalamu huru, imesema
kuwa Generali Amisi, anaendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa makundi
ya kihalifu na waasi wanaohudumu Mashariki mwa Congo, eneo ambao bado
kuna idadi kubwa ya wapiganaji wa waasi.
Hata
hivyo kundi hilo la M23 halikuwa miongoni mwa makundi yaliyotajwa
kwenye ripoti hiyo lakini kundi la Raia Mutomboki, moja ya makundi
kadhaa yanayojumuisha wapiganaji wa Mai Mai, inaaminika kuwa na
uhusiano wa karibu na kundi hilo la M23.
Ripoti
hiyo ya Umoja wa Mataifa imenadi kuwa Generali Amisi aliagiza bundi
300, aina ya AK-47 kukabithiwa kundi moja linalohudumu katika eneo hilo
la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lijulikanalo kama
Nyatura.
Ripoti hiyo imeongeza kusema kuwa
waasi hao wananunua risasi kutoka kwa nchi jirani ya Congo na
kusafirisha kupitia Kinshasa hado Mashariki mwa nchi hiyo na mtandao
unaoendeshwa na washirika wa Generali Amisi, wakiwemo baadhi ya jamaa
ya familia yake.
chanzo:bbc
0 comments:
Post a Comment