Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho akitia
saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mhashamu Baba Askofu Aloysius
Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga baada ya kuwasili kwenye Kanisa
la Mama wa Huruma katika Parokia ya Ngokolo mjini Shinyanga kushiriki
mazishi ya Askofu huyo, Jumamosi, Novemba 10, 2012.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mhashamu Baba Askofu Aloysious
Balina wa Jimbo Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi wa Askofu huyo
kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Ngokolo, mjini Shinyanga leo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wakati wa
mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, mjini
Shinyanga.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Aloysius Balina wa Jimbo
Katoliki la Shinyanga wakati wa mazishi ya Askofu huyo kwenye Kanisa la
Mama wa Huruma, Ngokolo, Shinyanga
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki kumzika
Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mhashamu Baba Askofu Aloysius
Balina yaliyofanyika kwenye Kanisa la Mama wa Huruma, Parokia ya
Ngokolo, mjini Shinyanga.
Rais
Kikwete ambaye amekwenda Shinyanga akitokea Dodoma ambako anaendesha
vikao muhimu vya Chama cha Mapinduzi amewasili kwenye Kanisa hilo kiasi
cha saa sita mchana kwa ajili ya mazishi ya Askofu Balina ambaye
alifariki dunia Novemba 6 mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa, Mwanza
kwa ugonjwa wa saratani.
Mara
baada ya kuwasili Kanisani hapo, Rais Kikwete ametia saini kitabu cha
maombolezo na kujiunga na viongozi wa Kanisa hilo na wa Serikali
akiwamo Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamin Mkapa na Mama Maria Nyerere
kushiriki katika mazishi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.
0 comments:
Post a Comment