.

.
Sunday, November 11, 2012

5:40 AM

Rais Kikwete akivishwa skafu na chipukizi wa CCM mjini Dodoma Picha kwa hisani ya Jiachie BlogNa Mwandishi Wetu,Dodoma
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete amesema kwamba migogoro ndani ya chama hicho inasababishwa na uroho wa vyeo na madaraka kiasi cha kusababisha vita kubwa ndani ya CCM.
Akizungumza na Wanachama CCM katika Mkutano Mkuu wa Nane wa chama hicho unaoendelea mjini Dodoma alisema, kuna watu  hodari wa kuwachukia wenzao kwa sababu tu wamekataa kuwaunga mkono ama wamekataa kuwaunga watu wao mkono..
“Migogoro ndani ya CCM inasababishwa na uroho wa madaraka,kwanini mgombane kwa kugombea uongozi, kwanini mtu achukiwe kwa kugombea uongozi, kwanini afanyiwe vitimbi, kwanini umchukie mtu aliyeamua kumuunga mkono mgombea mwingine, na kwanini umchukie aliyekataa kukuunga mkono wewe au kwa sababu amekataa kumuunga mkono mtu unayemtaka, tukiacha hayo hakuna mgogoro mwingine ndani ya chama niambieni”alisema Rais Kikwete na kuhoji.Nape akitumbuiza
Alisema “viongozi wenye chuki na bivu kubwa ndani ya Chama hicho ndiyo wenye tabia ya kuwa na andimi mbili na  kiongozi mwenye ndimi mbili hawafai ndani ya CCM kwa sababu akigeuka huku anasema ya CCM akigeuka huku anasema ya wengine, hivyo kuwa viongozi hao ndani ya CCM nisawa na kufuga nyoka ndani ya nyumba au mfukoni ambaye ukiingiza mkono tu mfukoni anakung’ata, bali tunataka kiongozi muadilifu na mwenye kuitendea haki chama na kutetea maslahi ya chama na mwenye uelewa mpana wa mambo ya chama”.
Katika hatua nyingine Rais Kikwete aliongeza kwamba uchaguzi wa viongozi uliopita katika Chama hicho ulikuwa na changamoto zake ambazo hawakuzizoea na wala hawakujiandaa kukutana nazo.
“Uchaguzi wa viongozi uliopita ndani ya CCM ulikuwa na changamoto ambazo hatukuzizoea na hatukujiandaa kukutana na nazo hivyo tukajikuta tuna wakati mgumu wa kufanya maamuzi yetu ya viongozi wetu lakini tumejifunza kutokana na hayo na tusikubali yajirudie katika chaguzi zetu”alifafanua Rais Kikwete.
chanzo http://www.habarimpya.com

0 comments:

Post a Comment