Di Matteo amebaki historia Chelsea |
BILIONEA Mrusi
Roman Abramovich amemfukuza kazi Kocha Mtaliano, Roberto Di Matteo asubuhi ya
leo baada ya matokeo mabaya mfululizo.
Mmiliki huyo
wa Chelsea, amekasirishwa na matokeo mabaya ya timu hiyo katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya, na kumfukuza kazi Mtaliano huyo baada ya timu kuzabwa mabao 3-0
na Juventus jana, ikiwa ni miezi sita tu tangu aipe timu hiyo taji la Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Sasa mtu wa
kwanza kabisa ambaye Abramovich anamtaka akarithi mikoba ya Mtaliano huyo ni
kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, na kama akikwama kwa Mspanyola
huyo ambaye amesema hataki ukocha tena kwa sasa, basi atahamishia ndoana zake
kwa Rafa Benitez.
MAKOCHA
WALIODUMU MUDA MFUPI CHESLEA:
Guus Hiddink
Siku
105
Felipe
Scolari Siku 223
Avram Grand Siku
247
Andre
Villas-Boas Siku 256
Roberto Di
Matteo Siku 262
MATOKEO YALIYOMFUKUZISHA
KAZI DI MATTEO:
Oktoba 23:
Shakhtar 2 Chelsea 1 (Ligi
ya Mabingwa)
Oktoba 28:
Chelsea 2 Man United 3 (Ligi Kuu)
Oktoba 31:
Chelsea 5 Man United 4 (Kombe
la Ligi)
Novemba 3:
Swansea 1 Chelsea 1 (Ligi
Kuu)
Novemba 7:
Chelsea 3 Shakhtar 2 (Ligi ya
Mabingwa)
Novemba 11:
Chelsea 1 Liverpool 1 (Ligi
Kuu)
Novemba 17:
West Brom 2 Chelsea 1 (Ligi Kuu)
Novemba 20:
Juventus 3 Chelsea 0 (Ligi ya Mabingwa)
...................xxx............xxx..................xxx...............
SUNZU KUENDELEA KUOGELEA KWENYE FWEZA MSIMBAZI
Feliux Sunzu akitibiwa |
Na Mahmoud Zubeiry
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. ataongezewa mkataba baada ya
kumaliza mkataba wake wa awali mwishoni mwa msimu katika klabu ya bingwa
Tanzania Bara, Simba SC.
Kiongozi
mmoja wa Simba amesema jana kwamba klabu hiyo
imeridhika na huduma ya mchezaji huyo mrefu na inahitaji kuendelea naye.
Kumekuwa na
mawazo tofauti ndani ya Simba SC kuhusu Sunzu, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji
anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Tanzania, Sh Milioni 5, kwamba hachezi kwa
kiwango cha fedha anazolipwa.
Lakini
wengine wanaamini Sunzu anawajibika vizuri na anastahili kwa fedha anayolipwa.
Pamoja na hayo, hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo kwa sasa, inatia shaka
kama itaweza kuurudia mkataba ule ule wa Sunzu.
Hata hivyo,
habari zaidi zinasema kwamba Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange
‘Kaburu’ ameamua kumaliza suala la Sunzu kwa kumsainisha mkataba mpya hivi
karibuni.
Baada ya
kumaliza mkataba wa awali, Simba ili kuendelea kuishi na Sunzu, inakadiriwa kumpa
fedha ya dau la usajili, ambalo kwa mwaka haliwezi kuwa chini ya dola za
Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. Milioni 20 za Tanzania) na kukubaliana kuhusu
mshahara uwe ule ule au mpya.
Kulingana
zengwe lililotawala juu ya dola za Kimarekani 3,500 anazolipwa Sunzu kuna
uwezekano Simba ikataka kuuteremsha mshahara huo, lakini habari zilizopatikana
jana zimesema kwamba Sunzu ataendelea kulipwa mshahara ule ule katika mkataba
wake mpya.
Kumalizika
kwa mkataba wa Sunzu ni mtihani mwingine kwa Simba, ambayo kwa sasa inakabiliwa
na kasheshe la kuingia mkataba mpya na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi
ambaye yuko vizuri kisoka na anatolewa macho na Azam na Yanga.
Na suala la
usajili linaonekana kuwa zito kwa wakati huu, kwa sababu Kamati ya Utendaji ya
Simba SC wiki hii imevunja Kamati zote ndogondogo, ikiwemo Kamati ya Usajili,
iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Zacharia Hans Poppe.
Hata hivyo,
inadaiwa vibopa wa Kamati ya Usajili, akiwemo Hans Poppe watarejeshewa majukumu
hayo.
................xxx......................xxx..........................xxx
MASHABIKI KANDA YA ZIWA WAENDA KUISAPOTI STARS KAMPALA
Frank Domayo, kiungo wa Kili Stars |
Na Mahmoud Zubeiry
UMOJA wa
wanamichezo waliowahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu ya Soka
Tanzania Bara wenye maskani yao mjini Bukoba, Kagera, Bukoba Veteran Sports
Club ni katika kuhamasisha ushiriki wa timu za Tanzania, Kilimanjaro
Stars na Zanzibar Heroes, kwenye michuano ya Kombe la Tusker Challenge
inayofanyika jijini Kampala Uganda, umeandaa safari ya mashabiki walioko mkoani
humo Kanda ya Ziwa kwa ujumla kwenda kushangilia mechi za timu hizo.
Katibu Mkuu
wa Bukoba Veterans, Shijja Richard ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba kwa
kuanzia, mashabiki hao wataondoka mjini Bukoba Jumapili Novemba 25, 2012 kwenda
kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika mechi
yake ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Sudan Kaskazini.
Amesema nia
na madhumuni ya safari hiyo ni kuhamasisha wachezaji wa timu za taifa za
Tanzania waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa kwenye ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati na kutoa hamasa kwa watanzania kujenga tabia ya
kushangilia timu zao na pia wanadhani kuwa ushiriki wao utaongeza ushindani
katika michuano hiyo.
Amesema tayari
taratibu zote zimeshafanyika ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Shirikisho la
Soka la Tanzania (TFF) ili wawasiliane na mamlaka zinazohusika kwa ajili ya
kupatiwa eneo maalumu uwanjani litakalowezesha watanzania waweze kuishangilia
vizuri timu ya taifa.
“Tunatarajia
kwenda uwanjani na zaidi ya mashabiki 60 ambao hivi sasa wanakamilisha taratibu
za mwisho za kuvuka mpaka wa nchi. Matarajio yetu ni kuendelea kuziunga mkono
timu za taifa katika michuano hiyo hadi kufikia mwisho wa michuano. Tunaomba
watanzania wengine walioko kanda ya ziwa katika mikoa ya Shinyanga, Mara na
Mwanza watuunge mkono,”alisema Richard.
Kikosi cha kinatarajiwa
kuwasili leo mjini Kampala, kikitokea Mwanza tayari kwa mashindano hayo ya
Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Tusker Challenge 2012
yanayotarajiwa kuanza kesho.
Stars
imekuwa kambini mjini Mwanza kwa takriban wiki mbili sasa ikijifua vikali chini
ya kocha wake, Mdenmark Kim Poulsen kujiandaa kwenda kutwaa taji la nne la
Challenge.
Kikosi cha
Kilimanjaro Stars kilichopo kambini mjini Mwanza, kinaundwa na makipa;
Juma Kaseja (Simba SC) na Deogratius Mushi ‘Dida’ wa Azam FC, mabeki; Kevin
Yondan (Yanga), Erasto Nyoni (Azam FC), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Shomari
Kapombe na Amir Maftah (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Amri Kiemba,
Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Mrisho Ngassa (Simba), Athuman
Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar) wakati washambuliaji
ni John Bocco ‘Adebayor’ (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Christopher Edward (Simba),
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa (TPM, DRC).
Bara ambayo inajivunia kutwaa mara tatu Kombe la Challenge
katika miaka ya 1974, 1994 na 2010 na kushika nafasi ya pili mara tano,
imepangwa Kundi B pamoja na Sudan, Burundi na Somalia.
Itaanza kampeni zake Novemba 25 kwa kumenyana na Sudan saa
12:00 jioni, mchezo utakaotanguliwa na mechi kati ya Burundi na Somalia
itakayoanza saa 9:00 Alasiri kabla ya kurudi tena dimbani, Novemba 28 kukipiga
na Burundi, mchezo utakaotanguliwa na mechi kati ya Somalia na Sudan.
Stars iatahitimisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na
Somalia Desemba 1, mchezo utakaotanguliwa na mechi nyingine kati ya Sudan na
Burundi. Mechi zote za Stars zitakuwa saa 12:00 jioni.
MAKUNDI
RATIBA TUSKER CHALLENGE 2012:
KUNDI A: Uganda,
Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini
KUNDI B: Tanzania,
Sudan, Burundi na Somalia
KUNDI C: Malawi,
Eritrea, Rwanda na Zanzibar
RATIB KUNDI
A:
Novemba 24, 2012:
Ethiopia v Sudan (Saa
9:00 Alasiri)
Uganda v Kenya (Saa 12:00 jioni)
Novemba 27, 2012:
Sudan Kusini v Kenya (Saa
9:00 Alasiri)
Uganda v Ethiopia (Saa
12:00 jioni)
Novemba 30, 2012:
Kenya v Ethiopia (Saa
9:00 Alasiri)
Sudan Kusini v Uganda (Saa
12:00 jioni)
RATIBA
KUNDI B:
Novemba 25, 2012:
Burundi v Somalia (Saa
9:00 Alasiri)
Tanzania v Sudan (Saa
12:00 jioni)
Novemba 28, 2012:
Somalia v Sudan (Saa
9:00 Alasiri)
Tanzania v Burundi (Saa
12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi (Saa
9:00 Alasiri)
Somalia v Tanzania (Saa
12:00 jioni)
RATIBA
KUNDI C:
Novemba 26, 2012:
Zanzibar v Eritrea (Saa
9:00 Alasiri)
Rwanda v Malawi (Saa
12:00 jioni)
Novemba 29, 2012:
Malawi v Eritrea (Saa
9:00 Alasiri)
Rwanda v Zanzibar (Saa
12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Malawi v Zanzibar (Saa
9:00 Alasiri)
Eritrea v Rwanda (Saa
12:00 jioni)
ROBO
FAINALI:
Desemba 3, 2012
Mshindi Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa
10:00 jioni)
Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa
1:00 usiku)
Desemba 4, 2012 (16:00):
Mshindi Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa
10:00 jioni)
Mshindi wa Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C (Saa 1:00 usiku)
NUSU
FAINALI:
Desemba 6, 2012
Nusu Fainali ya Kwanza (Saa
10:00 jioni)
Nusu Fainali ya Pili (Saa
1:00 usiku)
MSHINDI WA
TATU:
Desemba 8, 2012
Waliofungwa Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)
FAINALI:
Desemba 8, 2012
Walioshinda Nusu Fainali (Saa 1:00 usiku)
na Bin Zubery blog
0 comments:
Post a Comment