Wapiganaji
wa waasi wa M23, hatimaye wamefanikiwa kuingia mji mkuu wa eneo la
Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo lenye utajiri
mkubwa wa madini.
Mwandishi wa BBC mjini
Goma anasema wapiganaji hao wa waasi walikabiliana kwa risasi na
wanajeshi wa serikali, ambao walitoroka baada ya kuzidiwa nguvu.
Jeshi
la Umoja wa Matifa la Kutunza amani katika eneo hilo limekanusha madai
kuwa wapiganaji hao wa waasi wanathibiti uwanja wa NDEGE.
Maelfu
ya watu wametoroka makwao kufuatia mapigano hayo, ambayo yamezua wasi
wasi wa kuzuka upya kwa mapigano nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, mapigano ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu milioni
tano.
Hii ni mara ya kwanza tangu
kumalizika kwa mapigano mwaka wa 2003, ambapo wanajeshi wa waasi
wamefanikiwa kuingia mji huo wa Goma.
Takriban watu nusu milioni wanakadiriwa wanaishi mjini humo.
Takriban watu nusu milioni wanakadiriwa wanaishi mjini humo.
Serikali
ya Rwanda imekanusha madai ya mara kwa mara kutoka kwa serikali ya
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa inawaunga mkono wapiganaji hao
wa waasi wa M23.
Awali serikali ya
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilipuuzilia mbali makataa
iliyotolewa na wapiganaji wa waasi wa kuanzisha mazungumzo ya amani, na
kukariri kuwa itaendelea kuilinbda mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa umelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
chanzo :bbc
0 comments:
Post a Comment