.

.
Friday, November 16, 2012

10:08 AM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Kibo, Vincent Laswai akizungumza wakati wa hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa hoteli hiyo na kufanyika jijini Dar es Salaam.   
 Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba akizungumza wakati wa hafla maalum iliyoandaliwa na uongozi wa Kibo Palace Hotel ya Arusha  kwa ajili ya wateja wake na kufanyika jijini Dar es Salaam
 Meneja Maendeleo ya Biashara wa Hoteli ya Kibo, Charity Githinji akifafanua jambo wakati wa hafla maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa hoteli hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akiwa katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Kibo, Vincent Laswai akimkabidhi tiketi kwenda kulala katika hoteli ya Kibo, Kaimu Meneja Mauzo wa Precision Air, Ibrahim Bukenya wakati wa hafla iliyoandalkiwa na hoteli kwa ajili ya wateja wake na kufanyika jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washindi waliopata tiketi za kulala katika Hoteli ya Kibo

DAR ES SALAAM, Tanzania

Nina furaha Isiyo na kifani kwa kufika kwenu asubuhi hii, ingawa ni Siku ya kazi na Tumeandaa shughuli hii ambayo Inalenga wafanya maamuzi. Mimi na wenzangu tulidhani Tutakua na Watu Kama 50 tu. Lakini tulipotuma Mwaliko kwenu,tulipata majibu mazuri mno.

Kulingana mandhari ya kazi zangu, inawezekana kabisa isiwe rahisi kwa Mimi kukutana  nanyi  mnapokua mmeshukia hotelini au kuhudhuria shughuli mbalimbali Arusha. Ila ninapenda kuwahakikishia kuwa nina timu inayoniwakilisha na ninawafurahia sana.


Kama mlivyosikia kutoka kwa Charity kwamba, Hapo Kibo palace ilipojengwa ilikua Makao ya tembo. Na Kama ilivyo desturi ya tembo, nasi tunafuata nyayo hizo tukiwa na imani kuwa kama familia moja iliyo imara tunakuza biashara yetu tukiwa wamoja. Ninyi nyote mnatambua ya kuwa ili biashara zenu kukua na kuzalisha, lazima tuwe na umoja unaojumuisha kila mmoja wetu.



 Tembo ni kiiongozi, na tumedumisha uongozi Huo katika biashara yetu. Kibo palace inaongoza na tuna waahidi kuwa  tutabaki kuongoza na tutaendelea kuwapa huduma iliyo bora.

Mipango yetu ya baadae, ni kujikuza Kwenye secta ya utalii Kupitia kibo groups of companies. Tunatarajia Kuwa na ukumbi mkubwa wa mikutano Hapo Hapo ilipojengwa Kibo palace na utatoa huduma za kisasa ambazo hazipatikani katika Ukanda huo kwa vifaa vyake na huduma. Kwa wale wanaonifahamu Kati yenu wanajua ya kuwa ubora ni kila kitu katika kila jambo nilifanyalo. Nawahakikishia kuwa mtapata kilicho bora.



Mipango ya ngorongoro Kibo Lodge, Bado ipo na tunasubiri tu kibali ili tuendeleeze mipango hiyo. Tumechukua hatua mbalimbali na kutembelea hoteli za hathi mbalimbali ndani ya nchi na mataifa mengineyo, nawahakikishia kuwa,Ngorongoro patakua mahali pa kipekee tukiwa na cottages 50, huduma nzuri na pia chakula kizuri kama ambacho kimeifanya kibo palace kujulikana kwa ubora wake.



Kutokana na msingi wa Kibo palace hotel, Tunajitolea kwa Hali na Mali kusaidia Kwenye mfumo wa elimu na afya. Taifa litakuwa  bora kama tutajifunza kuchangia kwenye elimu na kuwa na Taifa  lililo na afya bora. Tuungane mikono   kusukuma gurudumu hili ili tuweze kuleta tofauti kwenye Jamii.


Nina timu inayojali na ninawatia moyo na kuwakuza.    Nikiwa  Kama mkurugenzi ninahakikisha kuwa wafanyakazi wangu wana furaha na mandhari  yao ya kazi . Ninaamini kuwa kampuni yoyote huanguka Ikiwa na wafanyakazi ambao hawafurahii kazi yaao.

Tuna mipango kabambe ambayo itatunufaisha Sisi sote, na leo kwa niaba ya timu iliyopo hapa na wale waliobaki arusha ni ombi langu kwenu kwamba ninawaomba muendelee kuiiunga mkono hoteli yetu na muwe huru kutusahihisha pale tunapokosea.



Nawatakieni wote pamoja na familia zenu sikukuu njema na mungu  awabariki Siku zote

0 comments:

Post a Comment