Serikali
ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imepuuzilia mbaya makataa
iliyotolewa na wapiganaji wa waasi wa kuanzisha mazungumzo ya amani, na
kukariri kuwa itaendelea kuilinbda mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi wa M23 wamesemekana kuukaribia mji huo huku maelfu ya raia wakikimbia makwao.
Mapema
hii leo, wapiganaji hao walitoa ilaani ya saa ishirini na manne kwa
serikali ya nchi hiyo kuanzisha mazungumzo, ya amani la sivyo
wataendelea na vita hivyo.
Baraza la usalama la umoja wa mataifa umelaaini hatua hiyo ya waasi wa M23 ya kuendelea na mapigano huku wakielekea mji wa Goma.
Mapigano hayo yametajwa kuwa mabaya zaidi tangu mwezi Julai Mwaka huu katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.
Barabaraza
mji wa Goma haikuwa na raia kama kawaida na magari ya kijeshi na yale
ya umoja wa mataifa ndiyo yaliyokuwa yakizunguka mji huo.
Waasi
hao wa M23 wamesema kuwa ikiwa serikali ya nchi hiyo haitakubali
kuanzisha mazungumzo hayo, hawatakuwa na budi ila kuendelea na mapigano
hayo, hadi watakapoiondoa utawala wa sasa.
Msemaji
wa serikali ya Congo Lambert Mende amesema waasi hao wanajumuisha
wanajeshi ambao wanaungwa mkono na serikali ya nchi jirani ya Rwanda,
ili kuficha vitendo vya kigaidi vinavyoendeleza katika eneo hilo la
Mashariki.
Lakini serikali ya Rwanda imepuuzilia mbali madai hayo, ikisema kuwa hayana msingi wowote.
0 comments:
Post a Comment