.

.
Thursday, November 22, 2012

4:59 AM

HATIMAYE madiwani watano  na Chama Cha Demokrasia na maendeleo(Chadema) wilayani Arusha ambao mnamo mwaka jana walitimuliwa kwa kosa la kumtabua meya wa Arusha  wamenusurika kwenda magereza baada ya hukumu ya  kesi ya madai iliyokuwa ikiwakabili kuamuru walipe kiasi cha sh,15 milioni kwa awamu mbili . 

Akitoa hukumu hiyo mbele ya umati wa watu ambao walikuwa wamefurika jana katika mahakama kuu kanda ya Arusha   hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Charles Magese alisema kuwa rufaa ya kesi dhidi yao imefika mwisho.

Magese, alisema kuwa washtakiwa hao ambao  walikuwa madiwani wa Chadema jijini  Arusha wamekutwa na hatia hivyo mahakama imeamuru walipe kiasi hicho cha fedha haraka iwezekanavyo na endapo wakishindwa kutekeleza agizo hilo hatua kali za kiesheria dhidi yao zitachukuliwa.

Aliongeza kuwa kwa sasa Madiwani hao wanatakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakuwa ndani ya wiki mbili kuanzia sasa wakati awamu ya pili itakuwa ya mwisho baada ya miezi miwili.

‘kwa sasa mnatakiwa muhakikishe kuwa mnalipa fidia kwa haraka kama mtashindwa kufanya hivyo basi mahakama itachukua hatua za kisheria zaidi’alisema Magese

Wakiongea nje ya mahakama hiyo kwa nyakati tofauti madiwai hao,Charles Mpanda”Rasta”,Rehema Mohammed na Ruben Ngowi walidai kwamba wote  wamekubaliana kulipa kiasi hicho
cha fedha lakini mengine wanamwachia Mungu.

Walidai kwamba wao wakati wakiwa madiwani walitumia nguvu na fedha zao za mifukoni kukitangaza chama hicho lakini leo wameambulia kufukuzwa kama yatima lakini wataendelea kupambana na siasa na hata kugombea udiwani kupitia milango mingine.

Awali Kesi hiyo ilitokana na madiwani hao kufungua kesi ya kupinga kufukuzwa na kuvuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukiuka sheria na kanuni za chama, zikiwemo sheria za kuwataka kutoingia katika vikao vya madiwani vya Jiji la Arusha kwa madai ya kutomtambua Meya wa Arusha Gaudence Lyimo wa Chama cha Mapinduzi(CCM).

MWISHO.

0 comments:

Post a Comment