.

.
Sunday, November 18, 2012

10:31 PM
Uganda, mabingwa wa kihistoria wa Challenge 

NA MAHMOUD ZUBEIRY
MICHUANO ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama CECAFA Challenge Cup, mwaka huu itafanyika mjini Kampala, Uganda kuanzia Novemba 24 hadi Desemba 8.
Kampuni ya Bia Afrika Mashariki (EABL), kupitia bia yake ya Tusker Lager, ndio wadhamini michuano hiyo kwa dau lao la dola za Kimarekani 450,000 walizitoa kwa ajili ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la CECAFA –Tusker Challenge Cup.
Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye alisema mapema tu wakati wa maandalizi ya awali ya michuano hiyo, kwamba lengo la michuano hiyo ni kuzisaidia maandalizi timu za Afrika Mashariki na Kati katika kuwania tiekti ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Udhamini wa mwaka huu huo ni ongezeko la aslimia 5, kutoka michuano ya mwaka jana mjini Dar es Salaam, ambayo Uganda waliibuka mabingwa.
Ni udhamini ambao utahusu usafiri, malazi na huduma nyingine, wakati jumla ya dola za Kimarekani 60.000 zitakuwa kwa ajili ya zawadi, bingwa akipewa dola 30.000, mshindi wa pili dola 20.000 na dola 10.000 mshindi wa tatu.   Kama ilivyo ada, mechi zote za michuano hiyo zitaonyeshwa na Televisheni ya Super Sport ya Afrika Kusini.
Michuano hiyo huandaliwa na CECAFA, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, ambalo lina wanachama 12.
Japokuwa ukanda wa CECAFA ndiyo eneo linalojikongoja kwa sasa katika soka ya kimataifa, lakini ukweli ni kwamba, mpira wa miguu barani Afrika, ulianzia ukanda wa Afrika Mashariki.
Michuano ya kwanza kabisa mikubwa barani Afrika, ilihusisha mataifa manne, Kenya, Uganda, Tanganyika (sasa Tanzania Bara) na Zanzibar, ikijulikana kwa jina la Kombe la Gossage.
Michuano hiyo ya Gossage ambayo sasa imekuwa Kombe la Challenge, ilifanyika mara 37 kuanzia mwaka 1926 hadi 1966, ilipobadilishwa jana na kuwa michuano ya wakubwa ya soka kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, ilifanyika mara saba kati ya mwaka 1965 na 1971, ilipozaliwa rasmi CECAFA Challenge.
Tanganyika ilianza kushiriki michuano hiyo tangu mwaka 1945, wakati Zanzibar ilijitosa miaka minne baadaye, 1949.
Michuano hiyo ilikuwa ikidhaminiwa na bepari aliyekuwa akimiliki kiwanda cha sabuni, William Gossage, aliyezaliwa Mei 12 mwaka 1799 na kufariki dunia Aprili 9, mwaka 1877.
Michuano hiyo mikongwe zaidi barani, imekuwa ikiandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ikihusisha timu za taifa za ukanda huo.
Hadi inafikia tamati michuano ya Gossage, Uganda ilikuwa inaongoza kwa kutwaa taji hilo, mara 22, ikifuatiwa na Kenya iliyotwaa mara 12 na Tanzania mara tano.
Mwaka 2005, michuano hiyo ilifanyika chini ya udhamini wa bilionea wa Ethiopia mwenye asili ya Saudi Arabia, Sheikh Mohammed Al Amoudi na kupewa jina la Al Amoudi Senior Challenge Cup, lakini sasa Tusker ndiyo mambo yote.

MABINGWA CHALLENGE;
Mwaka Bingwa         
1973    Uganda     
1974    Tanzania   
1975    Kenya      
1976    Uganda     
1977    Uganda     
1978    Malawi     
1979    Malawi     
1980    Sudan      
1981    Kenya      
1982    Kenya      
1983    Kenya      
1984    Zambia     
1985    Zimbabwe   
1986   Haikufanyika
1987    Ethiopia   
1988    Malawi     
1989    Uganda     
1990    Uganda     
1991    Zambia     
1992    Uganda     
1993   Haikufanyika
1994    Tanzania   
1995    Zanzibar   
1996    Uganda     
1997   Haikufanyika
1998   Haikufanyika    
1999    Rwanda B   
2000    Uganda     
2001    Ethiopia   
2002    Kenya      
2003    Uganda     
2004    Ethiopia   
2005    Ethiopia   
2006    Zambia     
2007    Sudan      
2009    Uganda     
2009    Uganda 
2010    Tanzania Bara
2011    Uganda

KUNDI A: Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini
KUNDI B: Tanzania, Sudan, Burundi na Somalia
KUNDI C: Malawi, Eritrea, Rwanda na Zanzibar

RATIB KUNDI A:
Novemba 24, 2012:
Ethiopia v Sudan               (Saa 9:00 Alasiri)
Uganda v Kenya                (Saa 12:00 jioni)
Novemba 27, 2012:
Sudan Kusini v Kenya       (Saa 9:00 Alasiri)
Uganda v Ethiopia             (Saa 12:00 jioni)
Novemba 30, 2012:
Kenya v Ethiopia               (Saa 9:00 Alasiri)
Sudan Kusini v Uganda     (Saa 12:00 jioni)

RATIBA KUNDI B:
Novemba 25, 2012:
Burundi v Somalia             (Saa 9:00 Alasiri)
Tanzania v Sudan              (Saa 12:00 jioni)
Novemba 28, 2012:
Somalia v Sudan                (Saa 9:00 Alasiri)
Tanzania v Burundi           (Saa 12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi                (Saa 9:00 Alasiri)
Somalia v Tanzania           (Saa 12:00 jioni)

RATIBA KUNDI C:
Novemba 26, 2012:
Zanzibar v Eritrea             (Saa 9:00 Alasiri)
Rwanda v Malawi             (Saa 12:00 jioni)
Novemba 29, 2012:
Malawi v Eritrea               (Saa 9:00 Alasiri)
Rwanda v Zanzibar           (Saa 12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Malawi v Zanzibar            (Saa 9:00 Alasiri)
Eritrea v Rwanda              (Saa 12:00 jioni)

ROBO FAINALI:
Desemba 3, 2012
Mshindi Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:00 jioni)
Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa 1:00 usiku)
Desemba 4, 2012 (16:00):
Mshindi Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa 10:00 jioni)
Mshindi wa Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C       (Saa 1:00 usiku)

NUSU FAINALI:
Desemba 6, 2012
Nusu Fainali ya Kwanza    (Saa 10:00 jioni)
Nusu Fainali ya Pili           (Saa 1:00 usiku)

MSHINDI WA TATU:
Desemba 8, 2012
Waliofungwa Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)

FAINALI:
Desemba 8, 2012
Walioshinda Nusu Fainali  (Saa 1:00 usiku)

0 comments:

Post a Comment