.

.
Wednesday, November 14, 2012

8:30 PM
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya  Sogea Satom ya nchini Ufaransa inayojenga barabara kati ya Arusha - Minjingu, mkoani Manyara wakiwa nje ya lango la Ofisi eneo la Kisongo, wilayani Arumeru mkoani Arusha jana,baada ya kugoma wakidai kupunjwa malipo na kufanya kazi zaidi ya muda wa kazi. Picha na Filbert Rweyemamu   
 
SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzindua ujenzi wa barabara ya Arusha hadi Minjingu, mkoani Manyara, wakati akiwa katika ziara yake katika mikoa ya kanda ya Kaskazini, jana wafanyakazi wa Kampuni  ya Sogea Satom inayokarabati barabara hiyo waligoma kufanya kazi.  
Wafanyakazi hao badala ya kwenda kwenye eneo la Nanja ambako kazi za ujenzi zinaendelea, waliamua kwenda zilipo ofisi za utawala eneo la Kisongo na kushinikiza walipwe stahili zao.

Mara baada ya uongozikubaini mgomo huo,Kampuni binafsi ya ulinzi ya KK Security iliongeza magari ili kuimarisha ulinzi eneo hilo.
Wafanyakazi walisema wanadai kupunjwa malipo yao kwa wasaidizi kutoka Sh7000 hadi 5000 huku wakifanya kazi saa 10 kwa siku badala ya saa 8 walizokubaliana na wakitakiwa kufanyakazi siku za Jumamosi na Jumapili bila malipo ya ziada.


“Hatuwezi kufanyakazi katika mazingira ya namna hii,huu ni unyanyasaji wa hali juu,Rais Kikwete alizindua barabara hii lakini  hata wiki mbili hazijaisha  tunanyanyaswa,”alisema Omary Athuman.


Mbali na kufanyakazi zaidi ya muda waliokubalina pia wanataka wapate ajira ya kudumu kwa maelezo kwamba wameshamaliza muda wa miezi mitatu kisheria wa kuwa vibarua.

Naye Innocent Bureta alidai Serikali na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inayowahudumia imekuwa kimya kuwaambia hatma ya madai yao wakati wao wanafanya kazi ngumu bila kupewa malipo ya muda wa ziada.


Wakati wafanyakazi hao wakizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Sakita Lekibelie alijaribu kuwazuia waandishi wa habari kufanyakazi zao hatua iliyopingwa na wafanyakazi na kuamua kurudi ofisini.


Jitihada za kuupata uongozi kuzungumzia madai ya wafanyakazi hazikufanikiwa baada ya Ofisa uhusiano kudai anayeweza kuzungumzia jambo hilo ni  meneja mradi ambaye hata hivyo hakuweza kupatikana kutokana na vikao vya dharura vilivyoitishwa.

Ukarabati wa barabara hiyo yenye kilometa 98 unagharamiwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya zaidi ya bii 75
 
chanzo cha habari :mwananchi

0 comments:

Post a Comment