.

.
Monday, November 5, 2012

9:59 AM
1
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza na Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband wakati ujumbe wa TTB ulipotembelea Uwanja wa Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya timu hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku ya jumamosi nchini Uingereza, Bodi ya utalii Tanzania inatangaza matangazo ya utalii wa Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika kuchezea ligi kuu ya Uingereza (Premier Liegue) kikiwemo kiwanja cha Sunderland FC, katika picha katikati ni Edmund Hazal Mkurugenzi wa Kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo,Bw. David Miliband pia ni mwenyekti wa klabu ya Sunderland. Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena kushoto mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya Suderland na Aston Villa, David Miliband pia ni mwenyekiti wa klabu ya SuderlandMkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani na maafisa wa timu ya Sunderland FC baada ya kukabidhiwa zawadi ya saa kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery, Gary Mutchinson Mkurugenzi wa Biashara na Kevin Ball Nahodha wa zamani wa timu hiyo.Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery kiutambulisha ujumbe wa maafisa wa bodi ya utalii TTB ulipotembelea uwanja huo.

1 comments:

  1. mdada mambo unafanya kazi nzuri but kumbuka kuweka bailaini za watu unaochukuwa stori kwao maana ipo siku zitakuletea matatizo ukichukuwa weka bailani umetoa wapi

    ReplyDelete